Ezekiel 14:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Tena nitauadhibu Yerusalemu kwa mapigo yangu manne ya hukumu kali: Vita, njaa, wanyama wakali na maradhi mabaya, niwatokomeze humo watu na wanyama!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Itakuwa vibaya kiasi gani nitakapopeleka dhidi ya Yerusalemu hukumu zangu nne za kutisha, yaani upanga, njaa, wanyama pori na tauni, ili kuua watu wake na wanyama wao!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Bwana MUNGU asema hivi; Je! U zaidi sana nitakapoleta hukumu zangu nne zilizo kali juu ya Yerusalemu, yaani, upanga, na njaa, na wanyama wabaya, na tauni, niwakatilie mbali nayo wanadamu na wanyama?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Tena nitauadhibu Yerusalemu kwa mapigo yangu manne ya hukumu kali: vita, njaa, wanyama wakali na maradhi mabaya, niwatokomeze humo watu na wanyama!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa maana hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Itakuwa vibaya kiasi gani nitakapopeleka dhidi ya Yerusalemu hukumu zangu nne za kutisha, yaani, upanga, njaa, wanyama pori na tauni, ili kuua watu wake na wanyama wao!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa maana hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Itakuwa vibaya kiasi gani nitakapopeleka dhidi ya Yerusalemu hukumu zangu nne za kutisha, yaani, upanga, njaa, wanyama pori na tauni, ili kuua watu wake na wanyama wao!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana Bwana MUNGU asema hivi; Je! U zaidi sana nitakapoleta hukumu zangu nne zilizo kali juu ya Yerusalemu, yaani, upanga, na njaa, na wanyama wabaya, na tauni, niwakatilie mbali nayo wanadamu na wanyama?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Tena nitauadhibu Yerusalemu kwa mapigo yangu manne ya hukumu kali: Vita, njaa, wanyama wakali na maradhi mabaya, niwatokomeze humo watu na wanyama!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Ingawa niupelekee Yerusalemu haya mapatilizo yangu manne yaliyo mabaya: panga na njaa na nyama wabaya na magonjwa mabaya, nitoweshe mwake watu na nyama,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana Bwana MUNGU asema hivi; Je! U zaidi sana nitakapoleta hukumu zangu nne zilizo kali juu ya Yerusalemu, yaani, upanga, na njaa, na wanyama wabaya, na tauni, niwakatilie mbali nayo wanadamu na wanyama?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Bwana wetu Yawe anasema: Tena nitauazibu Yerusalema kwa mapigo yangu mane ya hukumu kali: vita, njaa, nyama wakali na ugonjwa mukali, nipate kuangamiza watu na nyama ndani yake!