Ezekiel 14:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, sema nao uwaambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Mtu yeyote miongoni mwa Waisraeli anayekubali sanamu za miungu zimtawale moyoni, na kuiruhusu miungu hiyo kumwelekeza kutenda dhambi, kisha akaja kumwomba shauri nabii, atapata jibu kutoka kwangu ambalo litazifaa hata sanamu zake nyingi za miungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo sema nao uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mwisraeli yeyote anapoweka sanamu moyoni mwake na kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akaenda kwa nabii, Mimi Mwenyezi Mungu nitamjibu peke yangu sawasawa na ukubwa wa ibada yake ya sanamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sema nao, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Kila mtu wa nyumba ya Israeli atwaaye vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, na kumwendea nabii; mimi, Bwana, nitamjibu neno lake sawasawa na wingi wa sanamu zake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, sema nao uwaambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Mtu yeyote miongoni mwa Waisraeli anayekubali sanamu za miungu zimtawale moyoni, na kuiruhusu miungu hiyo kumwelekeza kutenda dhambi, kisha akaja kumwomba shauri nabii, atapata jibu kutoka kwangu ambalo litazifaa hata sanamu zake nyingi za miungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo sema nao uwaambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Wakati Mwisraeli ye yote anapoweka sanamu moyoni mwake na kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akaenda kwa nabii, Mimi BWANA nitamjibu peke yangu sawasawa na ukubwa wa ibada yake ya sanamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo sema nao uwaambie, ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Wakati Mwisraeli yeyote anapoweka sanamu moyoni mwake na kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akaenda kwa nabii, Mimi bwana nitamjibu peke yangu sawasawa na ukubwa wa ibada yake ya sanamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sema nao, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Kila mtu wa nyumba ya Israeli atwaaye vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, na kumwendea nabii; mimi, BWANA, nitamjibu neno lake kulingana na wingi wa sanamu zake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, sema nao uwaambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Mtu yeyote miongoni mwa Waisraeli anayekubali sanamu za miungu zimtawale moyoni, na kuiruhusu miungu hiyo kumwelekeza kutenda dhambi, kisha akaja kumwomba shauri nabii, atapata jibu kutoka kwangu ambalo litazifaa hata sanamu zake nyingi za miungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo sema nao na kuwaambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mtu ye yote wa mlango wa Isiraeli atakayeyatia magogo yake ya kutambikia moyoni mwake na kuyaweka mbele ya uso wake kuwa kwazo la kumkosesha, kisha akija kwa mfumbuaji, basi, mimi Bwana nitamjibu yayapasayo magogo yake mengi ya kutambikia,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sema nao, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Kila mtu wa nyumba ya Israeli atwaaye vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, na kumwendea nabii; mimi, BWANA, nitamjibu neno lake sawasawa na wingi wa sanamu zake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, sema nao uwaambie kwamba Bwana wao Yawe anasema: Mutu yeyote kati ya Waisraeli anayekubali sanamu za miungu zimutawale ndani ya moyo, na kuiruhusu miungu hiyo kumusukuma kutenda zambi, kisha akuje kumwomba nabii shauri, atapata jibu toka kwangu ambalo litafalia hata kwa sanamu zake nyingi za miungu.