Ezekiel 14:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Basi, waambie Waisraeli kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tubuni, na kuacha kuziabudu sanamu zenu za miungu. Acheni kufanya machukizo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Tubuni! Acheni sanamu zenu, na matendo yenu yote ya machukizo!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Rudini ninyi, mkageuke na kuviacha vinyago vyenu; mkageuze nyuso zenu zisielekee machukizo yenu yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Basi, waambie Waisraeli kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tubuni, na kuacha kuziabudu sanamu zenu za miungu. Acheni kufanya machukizo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Tubuni! Geukeni kutoka kwenye sanamu zenu na mkatae matendo yenu yote ya machukizo!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Tubuni! Geukeni kutoka kwenye sanamu zenu na mkatae matendo yenu yote ya machukizo!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Rudini ninyi, mkageuke na kuviacha vinyago vyenu; mkageuze nyuso zenu zisielekee machukizo yenu yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Basi, waambie Waisraeli kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tubuni, na kuacha kuziabudu sanamu zenu za miungu. Acheni kufanya machukizo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo waambie walio mlango wa Isiraeli: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Rudini! Jigeuzeni na kuyaacha magogo yenu ya kutambikia! Zigeuzeni nyuso zenu na kuyaacha machukizo yenu yote!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Rudini ninyi, mkageuke na kuviacha vinyago vyenu; mkageuze nyuso zenu zisielekee machukizo yenu yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, uwaambie Waisraeli kwamba: Bwana wetu Yawe anasema hivi: Munirudilie, na kuacha kuziabudu sanamu zenu za miungu. Muache kufanya machukizo.