Ezekiel 15:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitawakabili vikali. Hata kama wataukimbia moto, huo moto utawateketeza. Hapo nitakapowakabili vikali, ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitaukaza uso wangu dhidi yao. Ingawa watakuwa wameokoka kwenye moto, bado moto utawateketeza. Nitakapoukaza uso wangu dhidi yao, ninyi mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapoukaza uso wangu juu yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitawakabili vikali. Hata kama wataukimbia moto, huo moto utawateketeza. Hapo nitakapowakabili vikali, ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitaukaza uso wangu dhidi yao. Ingawa watakuwa wameokoka kwenye moto, bado moto utawateketeza. Nami nitakapoukaza uso wangu dhidi yao, ninyi mtajua kwamba Mimi ndimi BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitaukaza uso wangu dhidi yao. Ingawa watakuwa wameokoka kwenye moto, bado moto utawateketeza. Nami nitakapoukaza uso wangu dhidi yao, ninyi mtajua kwamba Mimi ndimi bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoukaza uso wangu juu yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitawakabili vikali. Hata kama wataukimbia moto, huo moto utawateketeza. Hapo nitakapowakabili vikali, ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitawakazia macho yangu: ijapo wametoka motoni, moto ndio utakaowala; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapowakazia macho yangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoukaza uso wangu juu yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawaazibu vikali. Hata kama wataukimbia moto, huo moto utawateketeza. Hapo nitakapowaazibu vikali, halafu mutatambua kwamba mimi ni Yawe.