Ezekiel 16:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, ukapambika kwa dhahabu na fedha. Vazi lako likawa la kitani safi na hariri, nalo lilikuwa limenakshiwa. Ulitumia unga safi, asali na mafuta kwa chakula chako. Ukawa mzuri kupindukia, ukaifikia hali ya kifalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; nguo zako zilikuwa za kitani safi, na hariri, na nguo iliyokuwa imetariziwa. Chakula chako kilikuwa unga laini, asali na mafuta ya zeituni. Ukawa mzuri sana, ukainuka kuwa malkia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikilia hali ya kifalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, ukapambika kwa dhahabu na fedha. Vazi lako likawa la kitani safi na hariri, nalo lilikuwa limenakshiwa. Ulitumia unga safi, asali na mafuta kwa chakula chako. Ukawa mzuri kupindukia, ukaifikia hali ya kifalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha, nguo zako zilikuwa za kitani safi, hariri na nguo iliyokuwa imetariziwa. Chakula chako kilikuwa unga laini, asali na mafuta ya zeituni. Ukawa mzuri sana ukainuka kuwa malkia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha, nguo zako zilikuwa za kitani safi, hariri na nguo iliyokuwa imetariziwa. Chakula chako kilikuwa unga laini, asali na mafuta ya zeituni. Ukawa mzuri sana ukainuka kuwa malkia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikia hali ya kifalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, ukapambika kwa dhahabu na fedha. Vazi lako likawa la kitani safi na hariri, nalo lilikuwa limenakshiwa. Ulitumia unga safi, asali na mafuta kwa chakula chako. Ukawa mzuri kupindukia, ukaifikia hali ya kifalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo ulipata mapambo ya dhahabu na ya fedha na mavazi ya bafta na ya hariri na ya nguo za rangi, ukala vikate vya unga uliopepetwa vema sana na asali na mafuta, ukawa mzuri sanasana, ukafanikiwa kupata macheo ya kifalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikilia hali ya kifalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, ukapambwa kwa zahabu na feza. Nguo yako ikakuwa ya kitani safi na hariri, nayo ilikuwa imepambwa. Ulitumia unga safi, asali na mafuta kwa chakula chako. Ukakuwa na sura nzuri sana, ukaifikia hali ya malkia.