Ezekiel 16:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Tena, watoto wako wa kiume na wa kike ulionizalia uliwatwaa, ukazitambikia sanamu zako kwa kuwateketeza. Je, unadhani uzinzi wako ulikuwa ni jambo dogo?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Nawe uliwachukua wanao wa kiume na wa kike ulionizalia na kuwatoa kafara kuwa chakula kwa sanamu. Je, ukahaba wako haukukutosha?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pamoja na hayo uliwatwaa wana wako na binti zako, ulionizalia, ukawatoa sadaka kwao ili waliwe. Je! Mambo yako ya kikahaba ni kitu kidogo tu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Tena, watoto wako wa kiume na wa kike ulionizalia uliwatwaa, ukazitambikia sanamu zako kwa kuwateketeza. Je, unadhani uzinzi wako ulikuwa ni jambo dogo?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Nawe uliwachukua wanao na binti zako ulionizalia mimi na kuwatoa kafara kuwa chakula kwa sanamu. Je, ukahaba wako haukukutosha?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Nawe uliwachukua wanao na binti zako ulionizalia mimi na kuwatoa kafara kuwa chakula kwa sanamu. Je, ukahaba wako haukukutosha?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Pamoja na hayo uliwatwaa wana wako na binti zako, ulionizalia, ukawatoa sadaka kwao ili waliwe. Je! Mambo yako ya kikahaba ni kitu kidogo tu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Tena, watoto wako wa kiume na wa kike ulionizalia uliwatwaa, ukazitambikia sanamu zako kwa kuwateketeza. Je, unadhani uzinzi wako ulikuwa ni jambo dogo?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukawachukua nao wanao wa kiume na wa kike, uliowazaa, wawe wangu, ukawatoa kuwa ng'ombe zao za tambiko na chakula chao. Je? Ugoni wako haukutosha,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pamoja na hayo uliwatwaa wana wako na binti zako, ulionizalia, ukawatoa sadaka kwao ili waliwe. Je! Mambo yako ya kikahaba ni kitu kidogo tu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, wana wako na wabinti zako ulionizalia uliwatwaa, ukawatambikia kwa sanamu zako wapate kukuliwa. Unazani uzinzi wako ulikuwa ni jambo dogo?