Ezekiel 16:31 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Umejijengea jukwaa lako mwanzoni mwa kila barabara na kujijengea mahali pa juu katika kila mtaa. Tena wewe hukuwa kama malaya kwani ulikataa kulipwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ulipojenga jukwaa lako katika mwanzo wa kila barabara, na kutengeneza mahali pako pa fahari pa ibada za sanamu katika kila kiwanja cha wazi, hukuwa kama kahaba, kwa sababu ulidharau malipo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
apendaye kutawala watu; kwa kuwa wajijengea mahali pako pakuu penye kichwa cha kila njia, na kufanya mahali pako palipoinuka katika kila njia kuu; lakini hukuwa kama kahaba, kwa maana ulidharau kupokea ujira.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Umejijengea jukwaa lako mwanzoni mwa kila barabara na kujijengea mahali pa juu katika kila mtaa. Tena wewe hukuwa kama malaya kwani ulikataa kulipwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Unapojenga jukwaa lako kila mwanzo wa barabara na kufanyiza mahali pa fahari pa ibada za miungu katika kila kiwanja cha wazi, lakini hukuwa kama kahaba, kwa sababu ulidharau malipo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Unapojenga jukwaa lako kila mwanzo wa barabara na kufanyiza mahali pa fahari pa ibada za miungu katika kila kiwanja cha wazi, lakini hukuwa kama kahaba, kwa sababu ulidharau malipo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
apendaye kutawala watu; kwa kuwa wajijengea mahali pako pakuu penye kichwa cha kila njia, na kufanya mahali pako palipoinuka katika kila njia kuu; lakini hukuwa kama kahaba, kwa maana ulidharau kupokea ujira.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Umejijengea jukwaa lako mwanzoni mwa kila barabara na kujijengea mahali pa juu katika kila mtaa. Tena wewe hukuwa kama malaya kwani ulikataa kulipwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ilikuwa hapo, ulipovojenga vyumba vyako vya vinyago po pote barabarani pembeni, ulipopatengeneza pako pa kutambikia uwanjani po pote. Tena hukuwa kama mwanamke mgoni aubeuaye mshahara.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
apendaye kutawala watu; kwa kuwa wajijengea mahali pako pakuu penye kichwa cha kila njia, na kufanya mahali pako palipoinuka katika kila njia kuu; lakini hukuwa kama kahaba, kwa maana ulidharau kupokea ujira.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umejijengea nafasi yako yenye kuinuka kwa mwanzo wa kila barabara na kujijengea pahali pa kutambikia katika kila kiwanja. Tena wewe haukukuwa kama kahaba maana ulikataa kulipwa.