Ezekiel 16:34 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika umalaya wako hukufanya kama wanawake wengine: Hakuna aliyekubembeleza ili uzini naye bali wewe ulilipa fedha badala ya kulipwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo wewe ulikuwa tofauti na wanawake wengine kwenye ukahaba wako. Hakuna aliyekutongoza ili kuzini naye, bali wewe ulikuwa tofauti kabisa, kwani ulilipa wakati hakuna malipo uliyolipwa wewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, katika mambo yako ya kikahaba, wewe na wanawake wengine ni mbalimbali, kwa kuwa hapana akufuataye katika mambo yako ya kikahaba; tena kwa kuwa unatoa ujira, wala hupewi ujira; basi, njia yako na njia yao ni mbalimbali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika umalaya wako hukufanya kama wanawake wengine: hakuna aliyekubembeleza ili uzini naye bali wewe ulilipa fedha badala ya kulipwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo wewe ulikuwa tofauti na wanawake wengine kwenye ukahaba wako, hakuna aliyekutongoza ili kuzini naye, wewe ndiye uliyelipa wakati hakuna malipo uliyolipwa wewe. Wewe ulikuwa tofauti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo wewe ulikuwa tofauti na wanawake wengine kwenye ukahaba wako, hakuna aliyekutongoza ili kuzini naye, wewe ndiye uliyelipa wakati hakuna malipo uliyolipwa wewe. Wewe ulikuwa tofauti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, katika mambo yako ya kikahaba, wewe na wanawake wengine ni mbalimbali, kwa kuwa hapana akufuataye katika mambo yako ya kikahaba; tena kwa kuwa unatoa ujira, wala hupewi ujira; basi, njia yako na njia yao ni tofauti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika umalaya wako hukufanya kama wanawake wengine: Hakuna aliyekubembeleza ili uzini naye bali wewe ulilipa fedha badala ya kulipwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwako, ukifanya ugoni, mambo yamegeuka, yasiwe kama kwa wanawake wengine: wewe hutakiwi ugoni wakikufuatafuata, ila huwapa mshahara wewe, usipewe mwenyewe mshahara; hivyo ndivyo, vilivyogeuka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, katika mambo yako ya kikahaba, wewe na wanawake wengine ni mbalimbali, kwa kuwa hapana akufuataye katika mambo yako ya kikahaba; tena kwa kuwa unatoa ujira, wala hupewi ujira; basi, njia yako na njia yao ni mbalimbali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika ukahaba wako haukufanya kama wanawake wengine: hakuna aliyekubembeleza kusudi uzini naye lakini wewe ulilipa feza pahali pa kulipwa.