Ezekiel 16:39 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitakutia mikononi mwa wapenzi wako, nao watabomoa jukwaa lako na mahali pako pa ibada. Watakuvua mavazi yako na kukunyanganya vito vyako, wakuache uchi, bila kitu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha nitakutia mikononi mwa wapenzi wako, nao watabomoa majukwaa yako na kuharibu mahali pako pa fahari pa ibada za sanamu. Watakuvua nguo zako na kuchukua vito vyako vya thamani na kukuacha uchi na bila kitu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena nitakutia katika mikono yao, nao watapaangusha mahali pako pakuu, na kupabomoa mahali pako palipoinuka, nao watakuvua nguo zako, na kutwaa vyombo vyako vya uzuri, nao watakuacha uchi, huna nguo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitakutia mikononi mwa wapenzi wako, nao watabomoa jukwaa lako na mahali pako pa ibada. Watakuvua mavazi yako na kukunyang'anya vito vyako, wakuache uchi, bila kitu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha nitakutia mikononi mwa wapenzi wako, nao watabomoa majukwaa yako na kuharibu mahali pako pa fahari pa ibada ya miungu. Watakuvua nguo zako na kuchukua vito vyako vya thamani na kukuacha uchi na bila kitu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha nitakutia mikononi mwa wapenzi wako, nao watabomoa majukwaa yako na kuharibu mahali pako pa fahari pa ibada ya miungu. Watakuvua nguo zako na kuchukua vito vyako vya thamani na kukuacha uchi na bila kitu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena nitakutia katika mikono yao, nao watapaangusha mahali pako pakuu, na kupabomoa mahali pako palipoinuka, nao watakuvua nguo zako, na kutwaa vyombo vyako vya uzuri, nao watakuacha uchi, bila mavazi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitakutia mikononi mwa wapenzi wako, nao watabomoa jukwaa lako na mahali pako pa ibada. Watakuvua mavazi yako na kukunyanganya vito vyako, wakuache uchi, bila kitu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena nitakutia mikononi mwao, wavivunje vyumba vyako vya vinyago, wapabomoe pako pa kutambikia, wakuvue nayo mavazi yako na kuyachukua mapambo yako matukufu, kisha wakuache, ukiwa mwenye uchi pasipo kujifunika kwa nguo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena nitakutia katika mikono yao, nao watapaangusha mahali pako pakuu, na kupabomoa mahali pako palipoinuka, nao watakuvua nguo zako, na kutwaa vyombo vyako vya uzuri, nao watakuacha uchi, huna nguo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitakutia katika mikono ya wapenzi wako, nao watabomoa nafasi yako yenye kuinuka na pahali pako pa kutambikia. Watakutosha nguo yako na kukunyanganya vitu vyako vya kujipamba, wakuache uchi, bila kitu.