Ezekiel 16:43 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe umesahau yale ambayo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nilikufanyia ulipokuwa kijana. Wewe umenichukiza mno kwa mambo hayo yote. Basi, nitakulipiza kisasi kuhusu kila kitu ulichotenda. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Je, hukuongeza uchafu juu ya machukizo yako yote?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Kwa sababu hukuzikumbuka siku za ujana wako, lakini ulinighadhibisha kwa mambo haya yote, hakika nitaleta juu ya kichwa chako yale uliyotenda, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Je, hukuongeza uasherati juu ya matendo yako mengine ya kuchukiza?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hukuzikumbuka siku za ujana wako, bali umenikasirisha kwa mambo hayo yote; basi, tazama, mimi nami nitaleta njia yako juu ya kichwa chako, asema Bwana MUNGU; wala hutafanya uasherati zaidi ya machukizo yako yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe umesahau yale ambayo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nilikufanyia ulipokuwa kijana. Wewe umenichukiza mno kwa mambo hayo yote. Basi, nitakulipiza kisasi kuhusu kila kitu ulichotenda. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Je, hukuongeza uchafu juu ya machukizo yako yote?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kwa sababu hukuzikumbuka siku za ujana wako, lakini ulinikasirisha kwa mambo haya yote, hakika nitaleta juu ya kichwa chako yale uliyotenda, asema BWANA Mwenyezi. Je hukuongeza uasherati juu ya matendo yako yote ya kuchukiza?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kwa sababu hukuzikumbuka siku za ujana wako, lakini ulinikasirisha kwa mambo haya yote, hakika nitaleta juu ya kichwa chako yale uliyotenda, asema bwana Mwenyezi. Je hukuongeza uasherati juu ya matendo yako yote ya kuchukiza?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hukuzikumbuka siku za ujana wako, bali umenikasirisha kwa mambo hayo yote; basi, tazama, mimi nami nitaleta matendo yako juu ya kichwa chako, asema Bwana MUNGU; wala hutafanya uasherati zaidi ya machukizo yako yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe umesahau yale ambayo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nilikufanyia ulipokuwa kijana. Wewe umenichukiza mno kwa mambo hayo yote. Basi, nitakulipiza kisasi kuhusu kila kitu ulichotenda. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Je, hukuongeza uchafu juu ya machukizo yako yote?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kuwa hukuzikumbuka siku za utoto wako, ukanichafua roho kwa kuyafanya hayo yote, kwa ajili ya hayo yote utaniona nami, nikikutwika njia yako kichwani; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu: Je? Hukuyaongeza machukizo yako yote kwa kufanya uzinzi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hukuzikumbuka siku za ujana wako, bali umenikasirisha kwa mambo hayo yote; basi, tazama, mimi nami nitaleta njia yako juu ya kichwa chako, asema Bwana MUNGU; wala hutafanya uasherati zaidi ya machukizo yako yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe umesahau yale ambayo mimi nilikufanyia ulipokuwa kijana. Wewe umenichukiza sana kwa mambo yale yote. Basi, nitakulipiza kisasi juu ya kila kitu ulichotenda. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe.– Haukuongeza uchafu juu ya machukizo yako yote?