Ezekiel 16:47 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wewe hukutosheka kufuata mienendo yao au kutenda sawa na machukizo yao. Kwa muda mfupi tu ulipotoka kuliko walivyopotoka wao katika mienendo yako yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hukuenda katika njia zao tu na kuiga matendo yao ya kuchukiza, bali baada ya muda mfupi, ulipotoka zaidi yao katika njia zako zote
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini hukuenda katika njia zao, wala hukutenda sawasawa na machukizo yao; lakini kana kwamba hilo ni jambo dogo sana, ulikuwa umeharibika kuliko wao katika njia zako zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wewe hukutosheka kufuata mienendo yao au kutenda sawa na machukizo yao. Kwa muda mfupi tu ulipotoka kuliko walivyopotoka wao katika mienendo yako yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hukuziendea njia zao tu na kuiga matendo yao ya kuchukiza, bali kwa muda mfupi katika njia zako zote uliharibika tabia zaidi kuliko wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hukuziendea njia zao tu na kuiga matendo yao ya kuchukiza, bali kwa muda mfupi katika njia zako zote uliharibika tabia zaidi kuliko wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini hukuenda katika njia zao, na hukutenda kulingana na machukizo yao; lakini kwa kitambo kidogo ulikuwa umepotoka kuliko wao katika njia zako zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wewe hukutosheka kufuata mienendo yao au kutenda sawa na machukizo yao. Kwa muda mfupi tu ulipotoka kuliko walivyopotoka wao katika mienendo yako yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe kwanza hukuzifuata njia zao, wala hukufanya machukizo kama yao. Lakini ilikuwa punje kidogo tu, kisha ukafanya mabaya yaliyo makuu kuliko yao katika njia zako zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini hukuenda katika njia zao, wala hukutenda sawasawa na machukizo yao; lakini kana kwamba hilo ni jambo dogo sana, ulikuwa umeharibika kuliko wao katika njia zako zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wewe haukutosheka kufuata mienendo yao au kutenda sawa na machukizo yao. Kwa muda mufupi tu ulipotoka kuliko vile wao walivyopotoka katika mienendo yako yote.