Ezekiel 16:51 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Samaria kwa kweli hakutenda hata nusu ya dhambi zako. Wewe umefanya machukizo mengi kuliko wao. Ukilinganisha maovu yako na ya dada zako, maovu yao si kitu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Samaria hakufanya hata nusu ya dhambi ulizofanya. Wewe umefanya mambo mengi sana ya kuchukiza kuwaliko, nawe umewafanya dada zako waonekane kama wenye haki kwa ajili ya mambo haya yote uliyoyafanya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Samaria naye hakutenda nusu ya dhambi zako; bali wewe umeyaongeza machukizo yako zaidi ya hao, nawe umewapa haki maumbu yako kwa machukizo yako yote uliyoyatenda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Samaria kwa kweli hakutenda hata nusu ya dhambi zako. Wewe umefanya machukizo mengi kuliko wao. Ukilinganisha maovu yako na ya dada zako, maovu yao si kitu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Samaria hakufanya hata nusu ya dhambi ulizofanya. Wewe umefanya mambo mengi sana ya kuchukiza kuliko wao, nawe umewafanya dada zako waonekane kama wenye haki kwa ajili ya mambo haya yote uliyofanya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Samaria hakufanya hata nusu ya dhambi ulizofanya. Wewe umefanya mambo mengi sana ya kuchukiza kuwaliko wao, nawe umewafanya dada zako waonekane kama wenye haki kwa ajili ya mambo haya yote uliyoyafanya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Samaria naye hakutenda nusu ya dhambi zako; bali wewe umeyaongeza machukizo yako zaidi ya hao, nawe umewapa haki dada zako kwa machukizo yako yote uliyoyatenda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Samaria kwa kweli hakutenda hata nusu ya dhambi zako. Wewe umefanya machukizo mengi kuliko wao. Ukilinganisha maovu yako na ya dada zako, maovu yao si kitu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Samaria makosa yake hayafiki kuwa nusu ya makosa yako wewe, ukayazidisha machukizo yako kuwa mengi kuliko yao; hivyo umetokeza, ya kuwa dada zako ni waongofu kuliko wewe kwa ajili ya machukizo yako yote, uliyoyafanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Samaria naye hakutenda nusu ya dhambi zako; bali wewe umeyaongeza machukizo yako zaidi ya hao, nawe umewapa haki maumbu yako kwa machukizo yako yote uliyoyatenda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Samaria kwa kweli hakutenda hata nusu ya zambi zako. Wewe umefanya machukizo mengi kuliko wao. Ukilinganisha maovu yako na ya dada zako, maovu yao si kitu!