Ezekiel 16:52 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe utaibeba aibu yako kabisa! Dhambi zako ni mbaya zaidi kuliko za dada zako, kiasi cha kuwafanya dada zako na dhambi zao waonekane hawana hatia. Basi, ona aibu na kubeba fedheha yako, maana umewafanya dada zako waonekane hawana hatia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Chukua aibu yako, kwa kuwa umefanya uovu wa dada zako uwe si kitu, nao waonekane kama wenye haki. Kwa kuwa dhambi zako zilikuwa mbaya kuliko zao, wameonekana wenye haki zaidi yako. Kwa hiyo basi, chukua aibu yako, kwa kuwa umewafanya dada zako waonekane wenye haki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wewe nawe, ichukue aibu yako mwenyewe, kwa kuwa umetoa hukumu juu ya maumbu yako; kwa dhambi zako ulizozitenda, zilizochukiza kuliko hao, wao wana haki kuliko wewe; naam, ufedheheke wewe nawe, ukaichukue aibu yako, kwa kuwa umewapa haki maumbu yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe utaibeba aibu yako kabisa! Dhambi zako ni mbaya zaidi kuliko za dada zako, kiasi cha kuwafanya dada zako na dhambi zao waonekane hawana hatia. Basi, ona aibu na kubeba fedheha yako, maana umewafanya dada zako waonekane hawana hatia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Chukua aibu yako, kwa kuwa umefanya uovu wa dada zako uwe si kitu, nao waonekane kama wenye haki. Kwa kuwa dhambi zako zilikuwa mbaya zaidi kuliko zao, wameonekana wenye haki zaidi kuliko wewe. Kwa hiyo basi, chukua aibu yako, kwa kuwa umewafanya dada zako waonekane wenye haki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Chukua aibu yako, kwa kuwa umefanya uovu wa dada zako uwe si kitu, nao waonekane kama wenye haki. Kwa kuwa dhambi zako zilikuwa mbaya zaidi kuliko zao, wameonekana wenye haki zaidi kuliko wewe. Kwa hiyo basi, chukua aibu yako, kwa kuwa umewafanya dada zako waonekane wenye haki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wewe nawe, ichukue aibu yako mwenyewe, kwa kuwa umetoa hukumu juu ya dada zako; kwa dhambi zako ulizozitenda, zilizochukiza kuliko hao, wao wana haki kuliko wewe; naam, ufedheheke wewe nawe, ukaichukue aibu yako, kwa kuwa umewapa haki dada zako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe utaibeba aibu yako kabisa! Dhambi zako ni mbaya zaidi kuliko za dada zako, kiasi cha kuwafanya dada zako na dhambi zao waonekane hawana hatia. Basi, ona aibu na kubeba fedheha yako, maana umewafanya dada zako waonekane hawana hatia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, wewe nawe shikwa na soni mwenyewe kama dada zako, ulipowaumbua! Kwa hivyo, ulivyokosa na kufanya machukizo kuliko wao, wameonekana kuwa waongofu kuliko wewe. Kwa hiyo wewe nawe iva uso kwa kushikwa na soni ikupasayo, kwa kuwa umewatokeza dada zako kuwa waongofu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wewe nawe, ichukue aibu yako mwenyewe, kwa kuwa umetoa hukumu juu ya maumbu yako; kwa dhambi zako ulizozitenda, zilizochukiza kuliko hao, wao wana haki kuliko wewe; naam, ufedheheke wewe nawe, ukaichukue aibu yako, kwa kuwa umewapa haki maumbu yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe utaibeba haya yako kabisa! Zambi zako ni mbaya zaidi kuliko za wadada zako, kwa kipimo cha kuwafanya wadada zako na zambi zao, waonekane kama hawana kosa. Basi, upate haya na kufezeheka, maana umewafanya wadada zako waonekane kama hawana kosa.