Ezekiel 16:55 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Dada zako, Sodoma na Samaria, pamoja na binti zao watairudia hali yao ya hapo awali. Hata wewe na binti zako mtairudia hali yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao dada zako, Sodoma na binti zake na Samaria na binti zake, watarudishwa kama vile walivyokuwa mwanzoni, nawe pamoja na binti zako mtarudishwa kama mlivyokuwa hapo awali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na maumbu yako, Sodoma na binti zake, watairudia hali yao ya kwanza, na Samaria na binti zake watairudia hali yao ya kwanza, na wewe na binti zako mtairudia hali yenu ya kwanza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Dada zako, Sodoma na Samaria, pamoja na binti zao watairudia hali yao ya hapo awali. Hata wewe na binti zako mtairudia hali yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao dada zako, Sodoma na binti zake na Samaria na binti zake, watarudishwa kama vile walivyokuwa mwanzoni, nawe pamoja na binti zako mtarudishwa kama mlivyokuwa hapo awali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao dada zako, Sodoma na binti zake na Samaria na binti zake, watarudishwa kama vile walivyokuwa mwanzoni, nawe pamoja na binti zako mtarudishwa kama mlivyokuwa hapo awali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na dada zako, Sodoma na binti zake, watairudia hali yao ya kwanza, na Samaria na binti zake watairudia hali yao ya kwanza, na wewe na binti zako mtairudia hali yenu ya kwanza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Dada zako, Sodoma na Samaria, pamoja na binti zao watairudia hali yao ya hapo awali. Hata wewe na binti zako mtairudia hali yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo dada zako Sodomu na wanawe watakapokuwa tena, kama walivyokuwa kale, naye Samaria na wanawe watakapokuwa tena, kama walivyokuwa kale, ndipo, wewe nawe na wanao mtakapokuwa, kama mlivyokuwa kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na maumbu yako, Sodoma na binti zake, watairudia hali yao ya kwanza, na Samaria na binti zake watairudia hali yao ya kwanza, na wewe na binti zako mtairudia hali yenu ya kwanza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wadada zako, Sodoma na Samaria, pamoja na wabinti zao watairudilia hali yao ya pale mbele. Hata wewe na wabinti zako mutairudilia hali yenu.