Ezekiel 17:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi Mwenyezi-Mungu naapa kwamba, kama niishivyo, mfalme huyu atafia katika nchi ya Babuloni, nchi ya mfalme yule aliyemweka awe mfalme, na ambaye amedharau kile kiapo na kuvunja lile agano alilofanya naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, atafia huko Babeli, katika nchi ya mfalme aliyemketisha kwenye kiti cha utawala, ambaye alidharau kiapo chake na kuvunja mapatano yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika mahali pale akaapo mfalme aliyemmilikisha, ambaye alikidharau kiapo chake, na kulivunja agano lake, ndipo atakapokufa pamoja naye kati ya Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi Mwenyezi-Mungu naapa kwamba, kama niishivyo, mfalme huyu atafia katika nchi ya Babuloni, nchi ya mfalme yule aliyemweka awe mfalme, na ambaye amedharau kile kiapo na kuvunja lile agano alilofanya naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Hakika kama niishivyo, asema BWANA Mwenyezi, atafia huko Babeli, katika nchi ya mfalme aliyemketisha katika kiti cha enzi, ambaye alidharau kiapo chake na kuvunja mapatano yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Hakika kama niishivyo, asema bwana Mwenyezi, atafia huko Babeli, katika nchi ya mfalme aliyemketisha katika kiti cha enzi, ambaye alidharau kiapo chake na kuvunja mapatano yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika mahali pale akaapo mfalme aliyemweka awe mfalme, ambaye alikidharau kiapo chake, na kulivunja agano lake, ndipo atakapokufa pamoja naye kati ya Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mimi Mwenyezi-Mungu naapa kwamba, kama niishivyo, mfalme huyu atafia katika nchi ya Babuloni, nchi ya mfalme yule aliyemweka awe mfalme, na ambaye amedharau kile kiapo na kuvunja lile agano alilofanya naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, kweli atakufa mle Babeli, mle mjini, mfalme akaamo aliyempa ufalme, kwa kuwa alikibeza kiapo chake na kulivunja agano lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika mahali pale akaapo mfalme aliyemmilikisha, ambaye alikidharau kiapo chake, na kulivunja agano lake, ndipo atakapokufa pamoja naye kati ya Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama vile ninavyoishi, mufalme huyu atakufia katika inchi ya Babeli, inchi ya mufalme yule aliyemuweka kuwa mufalme, na ambaye amezarau kile kiapo na kuvunja lile agano alilofanya naye.