Ezekiel 17:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitatandaza wavu wangu juu yake, naye atanaswa katika mtego wangu; nitampeleka mpaka Babuloni na kumhukumu kwa sababu ya uhaini alioufanya dhidi yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitautandaza wavu wangu kwa ajili yake, naye atanaswa katika mtego wangu. Nitamleta Babeli na kutekeleza hukumu juu yake huko kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitatandika wavu wangu juu yake, naye atanaswa katika mtego wangu, nami nitamleta hata Babeli; nami nitateta naye huko kwa sababu ya kosa lake alilonikosa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitatandaza wavu wangu juu yake, naye atanaswa katika mtego wangu; nitampeleka mpaka Babuloni na kumhukumu kwa sababu ya uhaini alioufanya dhidi yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitautandaza wavu wangu kwa ajili yake, naye atanaswa katika mtego wangu. Nitamleta mpaka Babeli na kutekeleza hukumu juu yake huko kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitautandaza wavu wangu kwa ajili yake, naye atanaswa katika mtego wangu. Nitamleta mpaka Babeli na kutekeleza hukumu juu yake huko kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitatandika wavu wangu juu yake, naye atanaswa katika mtego wangu, nami nitamleta hadi Babeli; nami nitateta naye huko kwa sababu ya kosa lake alilonikosa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitatandaza wavu wangu juu yake, naye atanaswa katika mtego wangu; nitampeleka mpaka Babuloni na kumhukumu kwa sababu ya uhaini alioufanya dhidi yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami nitamtegea wavu wangu, anaswe katika tanzi langu kisha nitampeleka Babeli; ndiko, nitakakomkatia shauri kwa kuyavunja maagano yangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitatandika wavu wangu juu yake, naye atanaswa katika mtego wangu, nami nitamleta hata Babeli; nami nitateta naye huko kwa sababu ya kosa lake alilonikosa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitatandaza wavu wangu juu yake, naye atanaswa katika mutego wangu; nitamupeleka mpaka Babeli na kumuhukumu kwa sababu ya udanganyifu alioufanya juu yangu.