Ezekiel 17:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo miti yote nchini itajua kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huiporomosha miti mirefu na kuikuza miti mifupi. Mimi hukausha miti mibichi na kustawisha miti mikavu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema hayo na nitayafanya.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Miti yote ya kondeni itajua kuwa Mimi Mwenyezi Mungu ninaishusha miti mirefu na kuikuza miti mifupi kuwa miti mirefu. Mimi naikausha miti mibichi na kuifanya miti mikavu istawi. “ ‘Mimi Mwenyezi Mungu nimesema, nami nitatenda.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na miti yote ya mashamba itajua ya kuwa mimi, Bwana, nimeushusha chini mti mrefu, na kuuinua mti mfupi, na kuukausha mti mbichi, na kuusitawisha mti mkavu; mimi, Bwana, nimenena, nami nimelitenda jambo hili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo miti yote nchini itajua kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huiporomosha miti mirefu na kuikuza miti mifupi. Mimi hukausha miti mibichi na kustawisha miti mikavu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema hayo na nitayafanya.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Miti yote ya kondeni itajua kuwa Mimi BWANA ninaishusha miti mirefu na kuikuza miti mifupi kuwa miti mirefu. Mimi naikausha miti mibichi na kuifanya miti mikavu istawi. “ ‘Mimi BWANA nimesema, nami nitatenda.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Miti yote ya kondeni itajua kuwa Mimi bwana ninaishusha miti mirefu na kuikuza miti mifupi kuwa miti mirefu. Mimi naikausha miti mibichi na kuifanya miti mikavu istawi. “ ‘Mimi bwana nimesema, nami nitatenda.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na miti yote ya mashamba itajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeushusha chini mti mrefu, na kuuinua mti mfupi, na kuukausha mti mbichi, na kuusitawisha mti mkavu; mimi, BWANA, nimenena, nami nimelitenda jambo hili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo miti yote nchini itajua kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huiporomosha miti mirefu na kuikuza miti mifupi. Mimi hukausha miti mibichi na kustawisha miti mikavu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema hayo na nitayafanya.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, miti yote ya shambani itakapojua, ya kuwa mimi Bwana hunyenyekeza mti mrefu, tena hukuza mti mfupi, ya kuwa mimi hukausha mti mbichi, tena huchipuza mti mkavu. Mimi Bwana niliyeyasema nitayafanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na miti yote ya mashamba itajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeushusha chini mti mrefu, na kuuinua mti mfupi, na kuukausha mti mbichi, na kuusitawisha mti mkavu; mimi, BWANA, nimenena, nami nimelitenda jambo hili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu miti yote katika inchi itajua kwamba mimi Yawe ninaishusha miti mirefu na kuinua miti mifupi. Mimi ninakausha miti mibichi na kustawisha miti yenye kukauka. Ni mimi Yawe ninayesema hayo na nitayafanya.