Ezekiel 17:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa; alikuwa na mabawa makubwa ya manyoya mengi. Basi, ule mzabibu ukamtandia mizizi yake, ukamwelekezea matawi yake, ili aumwagilie maji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa, mwenye mabawa yenye nguvu yaliyojaa manyoya. Tazama! Huu mzabibu ukatoa mizizi yake kumwelekea huyo tai kutoka mle kwenye shamba lile ulikopandwa, na kutanda matawi yake kumwelekea ili aunyweshe maji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kulikuwa na tai mwingine mkubwa, mwenye mabawa makubwa na manyoya mengi; na tazama, mzabibu huo ukapinda mizizi yake imwelekee yeye, ukachipuza matawi yake yamwelekee yeye, toka matuta yake ulipopandwa; ili yeye apate kuunywesha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa; alikuwa na mabawa makubwa ya manyoya mengi. Basi, ule mzabibu ukamtandia mizizi yake, ukamwelekezea matawi yake, ili aumwagilie maji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Lakini kulikuwapo na tai mwingine mkubwa, mwenye mabawa yenye nguvu yaliyojaa manyoya. Tazama! Huu mzabibu ukatoa mizizi yake kumwelekea huyo tai kutoka mle kwenye shamba lile ulikopandwa na kutanda matawi yake kumwelekea kwa ajili ya kupata maji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa, mwenye mabawa yenye nguvu yaliyojaa manyoya. Tazama! Huu mzabibu ukatoa mizizi yake kumwelekea huyo tai kutoka mle kwenye shamba lile ulikopandwa na kutanda matawi yake kumwelekea kwa ajili ya kupata maji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kulikuwa na tai mwingine mkubwa, mwenye mabawa makubwa na manyoya mengi; na tazama, mzabibu huo ukapinda mizizi yake imwelekee yeye, ukachipuza matawi yake yamwelekee yeye, toka matuta yake ulipopandwa; ili yeye apate kuunywesha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa; alikuwa na mabawa makubwa ya manyoya mengi. Basi, ule mzabibu ukamtandia mizizi yake, ukamwelekezea matawi yake, ili aumwagilie maji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kukawa na tai mkubwa mwingine mwenye mabawa makubwa yenye manyoya mengi; mara ule mzabibu ukampindukia yeye, mizizi yake imtwetee kwa kumtamani, nayo matawi yake ukamwelekezea yeye, aunyweshe kuliko hayo matuta, ulikopandwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kulikuwa na tai mwingine mkubwa, mwenye mabawa makubwa na manyoya mengi; na tazama, mzabibu huo ukapinda mizizi yake imwelekee yeye, ukachipuza matawi yake yamwelekee yeye, toka matuta yake ulipopandwa; ili yeye apate kuunywesha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kulikuwa tai mwingine mukubwa; alikuwa na mabawa makubwa ya manyoya mengi. Basi, ule muzabibu ulikunja mizizi yake, ukamwelekezea matawi yake, kusudi aumwangilie maji.