Ezekiel 18:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini nyinyi Waisraeli mwasema, ‘Anachotenda Mwenyezi-Mungu si sawa!’ Enyi Waisraeli, je, ninachofanya mimi si sawa? Mnachofanya nyinyi ndicho kisicho sawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini nyumba ya Israeli inasema, ‘Njia za Bwana si haki.’ Je, njia zangu si za haki, ee nyumba ya Israeli? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini nyumba ya Israeli husema, Njia ya Bwana si sawa. Ee nyumba ya Israeli, je! Njia zangu sizo zilizo sawa? Njia zenu sizo zisizo sawa?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini nyinyi Waisraeli mwasema, ‘Anachotenda Mwenyezi-Mungu si sawa!’ Enyi Waisraeli, je, ninachofanya mimi si sawa? Mnachofanya nyinyi ndicho kisicho sawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini nyumba ya Israeli inasema, ‘Njia za Bwana si haki.’ Je, njia zangu si za haki, Ee nyumba ya Israeli? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini nyumba ya Israeli inasema, ‘Njia za Bwana si haki.’ Je, njia zangu si za haki, ee nyumba ya Israeli? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini nyumba ya Israeli husema, Njia ya Bwana si sawa. Ee nyumba ya Israeli, je! Njia zangu sizo zilizo sawa? Njia zenu sizo zisizo sawa?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini nyinyi Waisraeli mwasema, ‘Anachotenda Mwenyezi-Mungu si sawa!’ Enyi Waisraeli, je, ninachofanya mimi si sawa? Mnachofanya nyinyi ndicho kisicho sawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wao wa mlango wa Isiraeli wakisema: Njia ya Bwana hainyoki, inakuwaje, njia zangu zisiponyoka? Ninyi wa mlango wa Isiraeli, sizo njia zenu zisizonyoka?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini nyumba ya Israeli husema, Njia ya Bwana si sawa. Ee nyumba ya Israeli, je! Njia zangu sizo zilizo sawa? Njia zenu sizo zisizo sawa?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninyi Waisraeli munasema: Anachotenda Yawe si sawa! Enyi Waisraeli, basi, ninachofanya mimi si sawa? Munachofanya ninyi ndicho kisichokuwa sawa.