Ezekiel 18:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kwa hiyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nasema hivi: Nitawahukumu nyinyi Waisraeli, kila mmoja wenu, kulingana na mwenendo wake. Tubuni na kuachana na makosa yenu, yasije yakawaangamiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hiyo, ee nyumba ya Israeli, nitawahukumu, kila mmoja sawasawa na njia zake, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Tubuni! Geukeni kutoka makosa yenu yote, ndipo dhambi haitakuwa anguko lenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, nitawahukumu ninyi, nyumba ya Israeli, kila mmoja kwa kadiri ya njia zake, asema Bwana MUNGU. Rudini, mkaghairi, na kuyaacha makosa yenu yote; basi hivyo uovu wenu hautakuwa uharibifu wenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kwa hiyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nasema hivi: Nitawahukumu nyinyi Waisraeli, kila mmoja wenu, kulingana na mwenendo wake. Tubuni na kuachana na makosa yenu, yasije yakawaangamiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa hiyo, Ee nyumba ya Israeli, nitawahukumu, kila mmoja sawasawa na njia zake, asema BWANA Mwenyezi. Tubuni! Geukeni kutoka katika makosa yenu yote, ndipo dhambi haitakuwa anguko lenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hiyo, ee nyumba ya Israeli, nitawahukumu, kila mmoja sawasawa na njia zake, asema bwana Mwenyezi. Tubuni! Geukeni kutoka makosa yenu yote, ndipo dhambi haitakuwa anguko lenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, nitawahukumu ninyi, nyumba ya Israeli, kila mmoja kwa kadiri ya njia zake, asema Bwana MUNGU. Rudini, mkaghairi, na kuyaacha makosa yenu yote; basi hivyo uovu wenu hautakuwa uharibifu wenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kwa hiyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nasema hivi: Nitawahukumu nyinyi Waisraeli, kila mmoja wenu, kulingana na mwenendo wake. Tubuni na kuachana na makosa yenu, yasije yakawaangamiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo nitawapatiliza ninyi wa mlango wa Isiraeli kila mtu, kama njia zakezilivyo; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu. Rudini na kujigeuza na kuyaacha mapotovu yenu yote, yasiwawie tena makwazo ya kuwakosesha!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, nitawahukumu ninyi, nyumba ya Israeli, kila mmoja kwa kadiri ya njia zake, asema Bwana MUNGU. Rudini, mkaghairi, na kuyaacha makosa yenu yote; basi hivyo uovu wenu hautakuwa uharibifu wenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, nitawahukumu ninyi Waisraeli, kila mumoja wenu, kulingana na mwenendo wake. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe.– Mugeuke na kuachana na makosa yenu yasipate kuwaangamiza.