Ezekiel 2:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akiniambia, “Wewe mtu nakutuma kwa Waisraeli, taifa la waasi ambao wameniasi. Wameendelea kunikosea mimi hadi leo kama walivyokuwa wazee wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaniambia: “Mwanadamu, ninakutuma kwa Waisraeli, taifa ambalo limeniasi mimi; wao na baba zao wameniasi hadi leo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaniambia, Mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi; wao na baba zao wamekosa juu yangu, naam, hata hivi leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akiniambia, “Wewe mtu nakutuma kwa Waisraeli, taifa la waasi ambao wameniasi. Wameendelea kunikosea mimi hadi leo kama walivyokuwa wazee wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaniambia: “Mwanadamu, ninakutuma kwa Waisraeli, kwa taifa asi ambalo limeniasi mimi, wao na baba zao wananikosea mimi hadi leo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaniambia: “Mwanadamu, ninakutuma kwa Waisraeli, kwa taifa asi ambalo limeniasi mimi, wao na baba zao wananikosea mimi hadi leo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaniambia, Mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi; wao na baba zao wameasi juu yangu, naam, hata hivi leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akiniambia, “Wewe mtu nakutuma kwa Waisraeli, taifa la waasi ambao wameniasi. Wameendelea kunikosea mimi hadi leo kama walivyokuwa wazee wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaniambia: Wewe mwana wa mtu, mimi ninakutuma kwa wana wa Isiraeli walio mataifa makatavu, walionikataa mimi, wao wenyewe na baba zao wamenikosea mpaka leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaniambia, Mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi; wao na baba zao wamekosa juu yangu, naam, hata hivi leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
akiniambia hivi: Wewe mwanadamu ninakutuma kwa Waisraeli, taifa la waasi ambao wameniasi. Wameendelea kunikosea mimi mpaka leo sawa vile babu zao walivyofanya.