Ezekiel 2:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakisikia au wasiposikia, maana wao ni watu waasi, walau watatambua kwamba nabii amekuwapo miongoni mwao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama watasikiliza au hawatasikiliza, kwa kuwa wao ni nyumba ya uasi, watajua nabii amekuwa miongoni mwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia, (maana ndio nyumba ya kuasi hao), hata hivyo watajua ya kuwa nabii amekuwako miongoni mwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakisikia au wasiposikia, maana wao ni watu waasi, walau watatambua kwamba nabii amekuwapo miongoni mwao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama watasikiliza au hawatasikiliza, kwa kuwa wao ni nyumba ya kuasi, watajua nabii amekuwa miongoni mwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama watasikiliza au hawatasikiliza, kwa kuwa wao ni nyumba ya kuasi, watajua nabii amekuwa miongoni mwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao, iwe watasikia au hawataki kusikia, (maana ndio nyumba ya kuasi hao), hata hivyo watajua ya kuwa nabii amekuwako miongoni mwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakisikia au wasiposikia, maana wao ni watu waasi, walau watatambua kwamba nabii amekuwapo miongoni mwao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao ikiwa wanasikia, au ikiwa wanaacha kusikia, kwani ndio mlango mkatavu, lakini watajua, ya kuwa yuko mfumbuaji katikati yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia, (maana ndio nyumba ya kuasi hao), hata hivyo watajua ya kuwa nabii amekuwako miongoni mwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakisikia au wakikataa kusikia, maana hao ni watu waasi, watatambua kwamba nabii yuko katikati yao.