Ezekiel 20:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Niliwapa pia Sabato zangu ziwe ishara kati yangu na wao, wapate kujua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu ninayewatakasa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia niliwapa Sabato zangu kama ishara kati yangu nao, ili wapate kujua kuwa Mimi Mwenyezi Mungu niliwafanya watakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, Bwana, ndimi niwatakasaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Niliwapa pia Sabato zangu ziwe ishara kati yangu na wao, wapate kujua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu ninayewatakasa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia niliwapa Sabato zangu kama ishara kati yangu nao, ili wapate kujua kuwa Mimi BWANA niliwafanya kuwa watakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia niliwapa Sabato zangu kama ishara kati yangu nao, ili wapate kujua kuwa Mimi bwana niliwafanya kuwa watakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena niliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, BWANA, ndimi niwatakasaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Niliwapa pia Sabato zangu ziwe ishara kati yangu na wao, wapate kujua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu ninayewatakasa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikawapa nazo siku zangu za mapumziko, ziwe kielekezo cha maagano, tuliyoyaagana mimi nao, wajue, ya kuwa mimi ni Bwana awatakasaye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, BWANA, ndimi niwatakasaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Niliwapa vilevile Sabato zangu zikuwe kitambulisho kati yangu na wao, wapate kujua kwamba mimi ni Yawe ninayewatakasa.