Ezekiel 20:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Sasa, wewe mtu, waambie Waisraeli kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Wazee wenu walinikufuru kila mara kwa kukosa uaminifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hiyo, mwanadamu, sema na watu wa Israeli na uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Katika jambo hili pia, baba zenu walinikufuru kwa kuniacha mimi:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Baba zenu wamenitukana kwa jambo hili, kwa kuwa wamekosa kosa juu yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Sasa, wewe mtu, waambie Waisraeli kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Wazee wenu walinikufuru kila mara kwa kukosa uaminifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa hiyo, mwanadamu, sema na watu wa Israeli na uwaambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Katika hili pia, baba zenu walinikufuru kwa kuniacha mimi:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hiyo, mwanadamu, sema na watu wa Israeli na uwaambie, ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Katika hili pia, baba zenu walinikufuru kwa kuniacha mimi:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Baba zenu wamenitukana kwa jambo hili, kwa kuwa wametenda kosa juu yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Sasa, wewe mtu, waambie Waisraeli kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Wazee wenu walinikufuru kila mara kwa kukosa uaminifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo sema na mlango wa Isiraeli, wewe mwana wa mtu, uwaambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Hata kwa neno hili baba zenu walinitukana, wakilivunja agano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Baba zenu wamenitukana kwa jambo hili, kwa kuwa wamekosa kosa juu yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, wewe mwanadamu, uwaambie Waisraeli kwamba: Bwana wetu Yawe anasema hivi: Wazee wenu walinikufuru kila mara kwa kukosa uaminifu.