Ezekiel 20:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana nilipowapeleka katika ile nchi niliyoapa kuwapa, kila walipoona kilima kirefu au miti ya majani mengi, walianza kutoa matambiko na tambiko zao na kunichokoza. Hukohuko walitoa tambiko za harufu nzuri na kumimina tambiko za kinywaji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilipowaleta katika nchi niliyokuwa nimeapa kuwapa na kuona kilima chochote kirefu au mti wowote wenye majani mengi, huko walitoa dhabihu zao, wakatoa sadaka ambazo zilichochea hasira yangu, wakafukiza uvumba wenye harufu nzuri na kumimina sadaka zao za kinywaji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana nilipokuwa nimekwisha kuwaingiza katika nchi ile, ambayo naliuinua mkono wangu kuwapa, wakati huo walipoona kila mlima mrefu, na kila mti wenye majani mengi, walitoa matoleo yao huko, na huko walitoa chukizo la sadaka zao, na huko walifanya nukato la kupendeza, na huko walimimina sadaka zao za kunywewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana nilipowapeleka katika ile nchi niliyoapa kuwapa, kila walipoona kilima kirefu au miti ya majani mengi, walianza kutoa matambiko na tambiko zao na kunichokoza. Hukohuko walitoa tambiko za harufu nzuri na kumimina tambiko za kinywaji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilipowaleta katika nchi ile ambayo nilikuwa nimeapa kuwapa na kuona kilima cho chote kirefu au mti wo wote wenye majani mengi, huko walitoa dhabihu zao, wakatoa sadaka ambazo zilichochea hasira yangu, wakafukiza uvumba wenye harufu nzuri na kumimina sadaka zao za kinywaji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilipowaleta katika nchi ile ambayo nilikuwa nimeapa kuwapa na kuona kilima chochote kirefu au mti wowote wenye majani mengi, huko walitoa dhabihu zao, wakatoa sadaka ambazo zilichochea hasira yangu, wakafukiza uvumba wenye harufu nzuri na kumimina sadaka zao za kinywaji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana nilipokuwa nimekwisha kuwaingiza katika nchi ile, ambayo niliuinua mkono wangu kuwapa, wakati huo walipoona kila mlima mrefu, na kila mti wenye majani mengi, walitoa matoleo yao huko, na huko walitoa chukizo la sadaka zao, na huko walifukiza manukato ya kupendeza, na huko walimimina sadaka zao za kunywewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana nilipowapeleka katika ile nchi niliyoapa kuwapa, kila walipoona kilima kirefu au miti ya majani mengi, walianza kutoa matambiko na tambiko zao na kunichokoza. Hukohuko walitoa tambiko za harufu nzuri na kumimina tambiko za kinywaji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipokuwa nimekwisha kuwapeleka katika nchi, niliyowaapia kwa kuuinua mkono wangu kwamba: Nitawapa basi, po pote walipoona kilima kirefu, napo walipoona mti wenye majani mengi, ndipo, walipochinja ng'ombe zao za tambiko, wakatoa hapohapo vipaji vyao vya tambiko, kusudi wanikasirishe, wakavukiza hapo uvumba wao wenye mnuko wa kupendeza, wakamwagia hapo vinywaji vyao vya tambiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana nilipokuwa nimekwisha kuwaingiza katika nchi ile, ambayo naliuinua mkono wangu kuwapa, wakati huo walipoona kila mlima mrefu, na kila mti wenye majani mengi, walitoa matoleo yao huko, na huko walitoa chukizo la sadaka zao, na huko walifanya nukato la kupendeza, na huko walimimina sadaka zao za kunywewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana nilipowapeleka katika ile inchi niliyoapa kuwapa, kila mara walipoona kilima kirefu au miti ya majani mengi, walianza kutoa matambiko na sadaka zao na kunichokoza. Kulekule walitoa sadaka za harufu nzuri na kutoa sadaka za kinywaji.