Ezekiel 20:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wewe mtu, sema na hao wazee wa Israeli. Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Je, mmekuja kuniuliza shauri? Hakika, kama niishivyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nasema kuwa sitakubali kuulizwa kitu na nyinyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mwanadamu, sema na wazee wa Israeli uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kwa nini mmekuja? Je, ni kutaka ushauri kwangu? Hakika kama niishivyo, sitawaruhusu mtake ushauri toka kwangu, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanadamu, sema na wazee wa Israeli, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Je! Mmekuja kuniuliza neno? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wewe mtu, sema na hao wazee wa Israeli. Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Je, mmekuja kuniuliza shauri? Hakika, kama niishivyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nasema kuwa sitakubali kuulizwa kitu na nyinyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mwanadamu, sema na wazee wa Israeli uwaambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Kwa nini mmekuja? Je, ni kutaka ushauri kwangu? Hakika kama niishivyo, sitawaruhusu mtake ushauri toka kwangu, asema BWANA Mwenyezi.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mwanadamu, sema na wazee wa Israeli uwaambie, ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Kwa nini mmekuja? Je, ni kutaka ushauri kwangu? Hakika kama niishivyo, sitawaruhusu mtake ushauri toka kwangu, asema bwana Mwenyezi.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanadamu, sema na wazee wa Israeli, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Je! Mmekuja kuniuliza neno? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wewe mtu, sema na hao wazee wa Israeli. Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Je, mmekuja kuniuliza shauri? Hakika, kama niishivyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nasema kuwa sitakubali kuulizwa kitu na nyinyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwana wa mtu, sema na wazee wa Kiisiraeli, uwaambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Inakuwaje, mkija kuniuliza? Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, siulizwi nanyi! ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanadamu, sema na wazee wa Israeli, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Je! Mmekuja kuniuliza neno? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe mwanadamu, sema na hao wazee wa Waisraeli. Uwaambie kwamba: Bwana wetu Yawe anasema hivi: Mumekuja kuniuliza shauri? Kama vile ninavyoishi, sitakubali kuulizwa shauri na ninyi. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe.–