Ezekiel 20:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnapoendelea kutoa tambiko zenu na kuwapitisha watoto wenu motoni mnajitia unajisi mpaka leo hii. Je, nitaulizwa shauri nanyi, enyi watu wa Israeli? Lakini, kama niishivyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu naapa kwamba sitakubali kuulizwa shauri nanyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mnapotoa matoleo yenu, yaani kutoa kafara watoto wenu motoni, mnaendelea kujinajisi na sanamu zenu zote hadi leo. Je, niulizwe ushauri na ninyi, ee nyumba ya Israeli? Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, mimi sitaulizwa ushauri na ninyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mtoapo matoleo yenu, na kuwapitisha watoto wenu motoni, je! Mnajitia unajisi kwa vinyago vyenu vyote hata leo? Na mimi je! Niulizwe neno nanyi, Enyi nyumba ya Israeli? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnapoendelea kutoa tambiko zenu na kuwapitisha watoto wenu motoni mnajitia unajisi mpaka leo hii. Je, nitaulizwa shauri nanyi, enyi watu wa Israeli? Lakini, kama niishivyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu naapa kwamba sitakubali kuulizwa shauri nanyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mnapotoa matoleo yenu, yaani, wana wenu kafara katika moto, mnaendelea kujinajisi na sanamu zenu zote hadi siku hii ya leo. Je, niulizwe neno na ninyi, Ee nyumba ya Israeli? Hakika kama niishivyo, asema BWANA Mwenyezi, mimi sitaulizwa neno na ninyi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mnapotoa matoleo yenu, yaani, wana wenu kafara katika moto, mnaendelea kujinajisi na sanamu zenu zote hadi siku hii ya leo. Je, niulizwe neno na ninyi, ee nyumba ya Israeli? Hakika kama niishivyo, asema bwana Mwenyezi, mimi sitaulizwa neno na ninyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mtoapo matoleo yenu, na kuwapitisha watoto wenu motoni, je! Mnajitia unajisi kwa vinyago vyenu vyote hata leo? Na mimi je! Niulizwe neno nanyi, Enyi nyumba ya Israeli? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnapoendelea kutoa tambiko zenu na kuwapitisha watoto wenu motoni mnajitia unajisi mpaka leo hii. Je, nitaulizwa shauri nanyi, enyi watu wa Israeli? Lakini, kama niishivyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu naapa kwamba sitakubali kuulizwa shauri nanyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata kwa kutoa vipaji vyenu vya tambiko, mkiwapitisha wana wenu motoni, mnajipatia uchafu na kuyatumikia magogo yenu yote ya kutambikia mpaka siku ya leo, sasa je? Mimi niulizwe nanyi mlio mlango wa Isiraeli? Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu: Hivyo nilivyo Mwenye uzima, sitaulizwa nanyi kabisa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mtoapo matoleo yenu, na kuwapitisha watoto wenu motoni, je! Mnajitia unajisi kwa vinyago vyenu vyote hata leo? Na mimi je! Niulizwe neno nanyi, Enyi nyumba ya Israeli? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munapoendelea kutoa sadaka zenu na kuwateketeza watoto wenu kwa moto munajichafua mpaka leo hii. Nitaulizwa shauri nanyi, enyi watu wa Israeli? Kama vile ninavyoishi, –ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe– sitakubali kuulizwa shauri nanyi.