Ezekiel 20:39 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Na sasa, enyi Waisraeli, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nawaambia hivi: Haya! Endeleeni kuziabudu sanamu zenu za miungu, kama hamnisikilizi; lakini mtalazimika kuacha kulikufuru jina langu takatifu kwa tambiko na sanamu zenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Kwenu ninyi, ee nyumba ya Israeli, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nendeni mkatumikie sanamu zenu, kila mmoja wenu! Lakini baadaye hakika mtanisikiliza mimi nanyi hamtalinajisi tena Jina langu takatifu, kwa matoleo yenu na sanamu zenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na katika habari zenu, enyi nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi, Enendeni, mkavitumikie vinyago vyenu kila mmoja wenu; na wakati wa baadaye pia, kama hamtaki kunisikiliza; lakini jina langu takatifu hamtalitia unajisi tena, kwa matoleo yenu, na kwa vinyago wenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Na sasa, enyi Waisraeli, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nawaambia hivi: Haya! Endeleeni kuziabudu sanamu zenu za miungu, kama hamnisikilizi; lakini mtalazimika kuacha kulikufuru jina langu takatifu kwa tambiko na sanamu zenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kwa habari zenu ninyi, Ee nyumba ya Israeli, hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Nendeni mkatumikie sanamu zenu, kila mmoja wenu! Lakini baadaye hakika mtanisikiliza mimi nanyi hamtalinajisi tena Jina langu takatifu, kwa matoleo yenu na sanamu zenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kwa habari zenu ninyi, ee nyumba ya Israeli, hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Nendeni mkatumikie sanamu zenu, kila mmoja wenu! Lakini baadaye hakika mtanisikiliza mimi nanyi hamtalinajisi tena Jina langu takatifu, kwa matoleo yenu na sanamu zenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na katika habari zenu, enyi nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi, Nendeni, mkavitumikie vinyago vyenu kila mmoja wenu; na wakati wa baadaye pia, kama hamtaki kunisikiliza; lakini jina langu takatifu hamtalitia unajisi tena, kwa matoleo yenu, na kwa vinyago vyenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Na sasa, enyi Waisraeli, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nawaambia hivi: Haya! Endeleeni kuziabudu sanamu zenu za miungu, kama hamnisikilizi; lakini mtalazimika kuacha kulikufuru jina langu takatifu kwa tambiko na sanamu zenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kwa ajili yenu mlio mlango wa Isiraeli Bwana Mungu anasema hivi: Haya! Nendeni kila mtu kuyatumikia magogo yenu ya kutambikia! Lakini siku za nyuma mtanisikiliza kabisa, msilitie jina la Patakatifu pangu tena uchafu kwa vipaji vyenu vya tambiko na kwa magogo yenu ya kutambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na katika habari zenu, enyi nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi, Enendeni, mkavitumikie vinyago vyenu kila mmoja wenu; na wakati wa baadaye pia, kama hamtaki kunisikiliza; lakini jina langu takatifu hamtalitia unajisi tena, kwa matoleo yenu, na kwa vinyago wenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na sasa, enyi Waisraeli, Bwana wenu Yawe anawaambia hivi: Muendelee kuziabudu sanamu zenu za miungu, kama hamunisikilizi; lakini mutalazimishwa kuacha kulikufuru jina langu takatifu kwa sadaka na sanamu zenu.