Ezekiel 20:40 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, katika mlima wangu mtakatifu, mlima mrefu wa Israeli, natamka mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nyinyi nyote watu wa Israeli mtanitumikia huko. Huko mimi nitawapokeeni na kungojea mniletee huko sadaka na tambiko zenu bora na matoleo mliyoyaweka wakfu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa katika mlima wangu mtakatifu, mlima mrefu wa Israeli, asema Bwana Mungu Mwenyezi, hapo katika nchi nyumba yote ya Israeli itanitumikia mimi, nami huko nitawakubali. Huko nitataka sadaka zenu na matoleo ya malimbuko yenu, pamoja na dhabihu zenu takatifu zote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana katika mlima wangu mtakatifu, katika mlima mrefu sana wa Israeli, asema Bwana MUNGU, ndiko watakakonitumikia nyumba yote ya Israeli, wote pia katika nchi ile; nami nitawatakabali huko, na huko nitataka matoleo yenu, na malimbuko ya dhabihu zenu, pamoja na vitu vyenu vitakatifu vyote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, katika mlima wangu mtakatifu, mlima mrefu wa Israeli, natamka mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nyinyi nyote watu wa Israeli mtanitumikia huko. Huko mimi nitawapokeeni na kungojea mniletee huko sadaka na tambiko zenu bora na matoleo mliyoyaweka wakfu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa katika mlima wangu mtakatifu, mlima mrefu wa Israeli, asema BWANA Mwenyezi, hapo katika nchi nyumba yote ya Israeli itanitumikia mimi, nami huko nitawakubali. Huko nitataka sadaka zenu na matoleo ya malimbuko yenu, pamoja na dhabihu zenu takatifu zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa katika mlima wangu mtakatifu, mlima mrefu wa Israeli, asema bwana Mwenyezi, hapo katika nchi nyumba yote ya Israeli itanitumikia mimi, nami huko nitawakubali. Huko nitataka sadaka zenu na matoleo ya malimbuko yenu, pamoja na dhabihu zenu takatifu zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana katika mlima wangu mtakatifu, katika mlima mrefu sana wa Israeli, asema Bwana MUNGU, ndiko watakakonitumikia nyumba yote ya Israeli, wote pia katika nchi ile; nami nitawatakabali huko, na huko nitataka matoleo yenu, na malimbuko ya dhabihu zenu, pamoja na vitu vyenu vitakatifu vyote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, katika mlima wangu mtakatifu, mlima mrefu wa Israeli, natamka mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nyinyi nyote watu wa Israeli mtanitumikia huko. Huko mimi nitawapokeeni na kungojea mniletee huko sadaka na tambiko zenu bora na matoleo mliyoyaweka wakfu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ndivyo, asemavyo Bwana: Katika mlima wangu mtakatifu utakaokuwa mlima mrefu wa Isiraeli ndiko, watakakonitumikia wao wa milango yote ya Isiraeli nazo nchi zake zote; tena ndiko, nitakakowapendeza nikitaka kuvipokea vipaji vyenu, mtakavyonitolea, nayo malimbuko yenu ya kunitambikia katika yote, mtakayonitakasia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana katika mlima wangu mtakatifu, katika mlima mrefu sana wa Israeli, asema Bwana MUNGU, ndiko watakakonitumikia nyumba yote ya Israeli, wote pia katika nchi ile; nami nitawatakabali huko, na huko nitataka matoleo yenu, na malimbuko ya dhabihu zenu, pamoja na vitu vyenu vitakatifu vyote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana, katika mulima wangu mutakatifu, mulima murefu wa Israeli, ninyi wote watu wa Israeli mutanitumikia kule. –Ni ujumbe wa Yawe.– Huko mimi nitawapokea na kungojea muniletee sadaka na matoleo yenu bora na matoleo iliyotakaswa.