Ezekiel 20:44 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu, wakati nitakapowatendea nyinyi sio kulingana na mwenendo wenu na matendo yenu mabaya, bali kwa heshima ya jina langu. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nanyi mtajua kuwa mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitakapowatendea kwa ajili ya Jina langu, wala si sawasawa na njia zenu mbaya na matendo yenu maovu, ee nyumba ya Israeli, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapokuwa nimetenda nanyi kwa ajili ya jina langu, si sawasawa na njia zenu mbaya, wala si sawasawa na matendo yenu mabovu, enyi nyumba ya Israeli, asema Bwana MUNGU.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu, wakati nitakapowatendea nyinyi sio kulingana na mwenendo wenu na matendo yenu mabaya, bali kwa heshima ya jina langu. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nanyi mtajua kuwa mimi ndimi BWANA, nitakaposhughulika nanyi kwa ajili ya Jina langu na wala si sawasawa na njia zenu mbaya na matendo yenu maovu, Ee nyumba ya Israeli, asema BWANA Mwenyezi.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nanyi mtajua kuwa mimi ndimi bwana, nitakaposhughulika nanyi kwa ajili ya Jina langu na wala si sawasawa na njia zenu mbaya na matendo yenu maovu, ee nyumba ya Israeli, asema bwana Mwenyezi.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapokuwa nimetenda nanyi kwa ajili ya jina langu, si kulingana na njia zenu mbaya, wala si kulingana na matendo yenu maovu, enyi nyumba ya Israeli, asema Bwana MUNGU.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu, wakati nitakapowatendea nyinyi sio kulingana na mwenendo wenu na matendo yenu mabaya, bali kwa heshima ya jina langu. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapowafanyizia hivyo kwa ajili ya Jina langu, lakini sivyo kwa ajili ya njia zenu mbaya, wala kwa ajili ya matendo yenu maovu, ninyi wa mlango wa Isiraeli; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapokuwa nimetenda nanyi kwa ajili ya jina langu, si sawasawa na njia zenu mbaya, wala si sawasawa na matendo yenu mabovu, enyi nyumba ya Israeli, asema Bwana MUNGU.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu mutatambua kwamba mimi ni Yawe, wakati nitakapowatendea ninyi sio kulingana na mwenendo wenu na matendo yenu mabaya, lakini kwa heshima ya jina langu. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe.