Ezekiel 21:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe mtu, lia na kuomboleza upanga huo umenyoshwa dhidi ya watu wangu, dhidi ya wakuu wote wa Israeli. Wataangamizwa kwa upanga pamoja na watu wangu. Jipige kifua kwa huzuni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Piga kelele na uomboleze, ee mwanadamu, kwa kuwa upanga u dhidi ya watu wangu; u dhidi ya wakuu wote wa Israeli. Wametolewa wauawe kwa upanga pamoja na watu wangu. Kwa hiyo pigapiga kifua chako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Piga kelele, utoe sauti ya uchungu, Ee mwanadamu, kwa maana upanga u juu ya watu wangu, u juu ya wakuu wote wa Israeli; wametolewa wauawe na upanga pamoja na watu wangu, basi, jipige pajani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe mtu, lia na kuomboleza upanga huo umenyoshwa dhidi ya watu wangu, dhidi ya wakuu wote wa Israeli. Wataangamizwa kwa upanga pamoja na watu wangu. Jipige kifua kwa huzuni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Piga kelele na uomboleze, Ee mwanadamu, kwa kuwa upanga u dhidi ya watu wangu; u dhidi ya wakuu wote wa Israeli. Wametolewa wauawe kwa upanga pamoja na watu wangu. Kwa hiyo pigapiga kifua chako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Piga kelele na uomboleze, ee mwanadamu, kwa kuwa upanga u dhidi ya watu wangu; u dhidi ya wakuu wote wa Israeli. Wametolewa wauawe kwa upanga pamoja na watu wangu. Kwa hiyo pigapiga kifua chako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Piga kelele, utoe sauti ya uchungu, Ee mwanadamu, kwa maana upanga u juu ya watu wangu, u juu ya wakuu wote wa Israeli; wametolewa wauawe na upanga pamoja na watu wangu, basi, jipige pajani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe mtu, lia na kuomboleza upanga huo umenyoshwa dhidi ya watu wangu, dhidi ya wakuu wote wa Israeli. Wataangamizwa kwa upanga pamoja na watu wangu. Jipige kifua kwa huzuni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Piga yowe na kupaza sauti, mwana wa mtu! Kwani huo ndio unaowajia walio ukoo wangu, ndio unaowajia nao wakuu wa Isiraeli; wametupwa kwenye upanga pamoja nao walio ukoo wangu. Kwa hiyo jipige mapaja!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Piga kelele, utoe sauti ya uchungu, Ee mwanadamu, kwa maana upanga u juu ya watu wangu, u juu ya wakuu wote wa Israeli; wametolewa wauawe na upanga pamoja na watu wangu, basi, jipige pajani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakikuuliza hivi: Kwa nini unaomboleza? Utawaambia: Ninaomboleza kwa sababu ya habari zinazokuja. Kila mutu atavunjika moyo, mikono yao yote itaregea; kila mutu anayeishi atazimia na magoti yao yataregea. Habari hizo zinakuja kweli, nazo zinatimia. –Ni Bwana wetu Yawe anayesema hivyo.