Ezekiel 21:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo wamekufa moyo na wengi wanaanguka. Ncha ya upanga nimeiweka katika malango yao yote. Umefanywa ungae kama umeme, umengarishwa kwa ajili ya mauaji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ili mioyo ipate kuyeyuka na wanaouawa wawe wengi, nimeweka upanga wa mauaji kwenye malango yao yote. Lo! Umetengenezwa umetemete kama miali ya radi, umeshikwa kwa ajili ya kuua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nimeweka ncha ya upanga huo juu ya malango yao yote, ili mioyo yao iyeyuke, yakaongezeke makwazo yao; aha! Umefanywa kuwa kama umeme, umenolewa, ili uchinje.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo wamekufa moyo na wengi wanaanguka. Ncha ya upanga nimeiweka katika malango yao yote. Umefanywa ung'ae kama umeme, umeng'arishwa kwa ajili ya mauaji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ili mioyo ipate kuyeyuka na wanaouawa wawe wengi, nimeweka upanga wa kuchinja kwenye malango yao yote. Lo! Umetengenezwa umetemete kama umeme wa radi, umeshikwa kwa ajili ya kuua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ili mioyo ipate kuyeyuka na wanaouawa wawe wengi, nimeweka upanga wa kuchinja kwenye malango yao yote. Lo! Umetengenezwa umetemete kama umeme wa radi, umeshikwa kwa ajili ya kuua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nimeweka ncha ya upanga huo juu ya malango yao yote, ili mioyo yao iyeyuke, yakaongezeke makwazo yao; aha! Umefanywa kuwa kama umeme, umenolewa, ili uchinje.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo wamekufa moyo na wengi wanaanguka. Ncha ya upanga nimeiweka katika malango yao yote. Umefanywa ungae kama umeme, umengarishwa kwa ajili ya mauaji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kusudi mioyo iyeyuke, tena wengi waanguke kwa kukwazwa; malangoni pao po pote nitatoa matisho ya huo upanga. A! Umefanywa, umerimete kama umeme! Umenolewa, upate kuchinja!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nimeweka ncha ya upanga huo juu ya malango yao yote, ili mioyo yao iyeyuke, yakaongezeke makwazo yao; aha! Umefanywa kuwa kama umeme, umenolewa, ili uchinje.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umenolewa kusudi ufanye mauaji, umeangarishwa umetemete kama umeme!