Ezekiel 21:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mshale unaodokezea ‘Yerusalemu’ umeangukia mkono wake wa kulia. Anaweka zana za kubomolea, anaamuru mauaji na kelele za vita zifanywe, zana za kubomolea malango zimewekwa, maboma na minara ya kuuzingira mji vimewekwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Upande wake wa kuume inakuja kura ya Yerusalemu, ambapo ataweka magogo ya kubomoa, ili kuamrisha mauaji, kupiga ukelele wa vita, kuweka magogo ya kubomoa dhidi ya malango, kupandisha kilima hadi kuta zako, na kujenga husuru dhidi yako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika mkono wake wa kuume alikuwa na kura ya Yerusalemu, kuviweka vyombo vya kubomolea, kufumbua kinywa katika machinjo, kuiinua sauti kwa kupiga kelele sana, kuweka vyombo vya kubomolea juu ya malango, kufanya maboma, na kujenga ngome.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mshale unaodokezea ‘Yerusalemu’ umeangukia mkono wake wa kulia. Anaweka zana za kubomolea, anaamuru mauaji na kelele za vita zifanywe, zana za kubomolea malango zimewekwa, maboma na minara ya kuuzingira mji vimewekwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Upande wake wa kuume inakuja kura ya Yerusalemu, ambapo ataweka vyombo vya kuvunjia boma, ili kuamrisha mauaji, kupiga ukelele wa vita, kuweka vyombo vya kuvunjia boma kwenye malango, kuweka jeshi kuzunguka na kufanya uzingiraji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Upande wake wa kuume inakuja kura ya Yerusalemu, ambapo ataweka vyombo vya kuvunjia boma, ili kuamrisha mauaji, kupiga ukelele wa vita, kuweka vyombo vya kuvunjia boma kwenye malango, kuweka jeshi kuzunguka na kufanya uzingiraji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika mkono wake wa kulia alikuwa na kura ya Yerusalemu, kuviweka vyombo vya kubomolea, kufumbua kinywa katika machinjo, kuiinua sauti kwa kupiga kelele sana, kuweka vyombo vya kubomolea juu ya malango, kufanya maboma, na kujenga ngome.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mshale unaodokezea ‘Yerusalemu’ umeangukia mkono wake wa kulia. Anaweka zana za kubomolea, anaamuru mauaji na kelele za vita zifanywe, zana za kubomolea malango zimewekwa, maboma na minara ya kuuzingira mji vimewekwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kuumeni kwake kutaanguka kura ya Yerusalemu kwamba: aweke magogo ya kuvunjia boma, afumbue kinywa kupiga kelele, apaze sauti kupiga yowe, aweke magogo ya kuvunjia penye malango, azungushe ukingo wa mchanga, ajenge minara.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika mkono wake wa kuume alikuwa na kura ya Yerusalemu, kuviweka vyombo vya kubomolea, kufumbua kinywa katika machinjo, kuiinua sauti kwa kupiga kelele sana, kuweka vyombo vya kubomolea juu ya malango, kufanya maboma, na kujenga ngome.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nami nitapiga mikono, kasirani yangu itatosheka. Ni mimi Yawe ninayesema hivyo.