Ezekiel 21:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati nyinyi mmetulia katika maono yenu madanganyifu na utabiri wenu wa uongo, upanga utakuwa tayari kukata shingo za waasi na waovu. Siku imewadia ambapo maovu yenu yataadhibiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati wanatoa maono ya uongo juu yako, na wanapobashiri uongo juu yako, upanga utawekwa kwenye shingo za wapotovu watakaouawa, wale siku yao imewadia, wakati wa adhabu yao ya mwisho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakati wakuoneapo ubatili, wakati wakufanyiao uganga wa uongo, ili kukuweka juu ya shingo zao waliotiwa jeraha kiasi cha kuwaua, ambao siku yao imekuja, katika wakati wa uovu wa mwisho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati nyinyi mmetulia katika maono yenu madanganyifu na utabiri wenu wa uongo, upanga utakuwa tayari kukata shingo za waasi na waovu. Siku imewadia ambapo maovu yenu yataadhibiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wakitoa maono ya uongo kwa ajili yako, wanapobashiri uongo kwa ajili yako, wanakuweka wewe kwenye shingo za watu wapotovu, wale walio waovu, wale ambao siku yao imewadia, wakati wa adhabu yao ya mwisho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wakitoa maono ya uongo kwa ajili yako, wanapobashiri uongo kwa ajili yako, wanakuweka wewe kwenye shingo za watu wapotovu, wale walio waovu, wale ambao siku yao imewadia, wakati wa adhabu yao ya mwisho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakati wanapokupa maono ya udanganyifu, wakati wanapokuagulia uongo, wanakuweka juu ya shingo zao wachukizao, na waovu, ambao siku yao imekuja, katika wakati wa adhabu ya mwisho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati nyinyi mmetulia katika maono yenu madanganyifu na utabiri wenu wa uongo, upanga utakuwa tayari kukata shingo za waasi na waovu. Siku imewadia ambapo maovu yenu yataadhibiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wamekutazamia maono yasiyokuwa, wakakuagulia uwongo, wakuvute, uje kuwapiga shingo zao waliojipatia uchafu na kuacha kunicha, kwamba siku yao imetimia, kwa kuwa ni wakati wa mwisho wa kukora manza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakati wakuoneapo ubatili, wakati wakufanyiao uganga wa uongo, ili kukuweka juu ya shingo zao waliotiwa jeraha kiasi cha kuwaua, ambao siku yao imekuja, katika wakati wa uovu wa mwisho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, Bwana wetu Yawe anasema hivi: Wote wataweza kuziona zambi zenu. Kila mutu atajua jinsi munavyokuwa na makosa. Kila kitendo munachotenda kinaonyesha zambi zenu. Ninyi mutapata azabu nami nitawatia katika mikono ya waadui zenu.