Ezekiel 22:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wewe mtu! Waambie Waisraeli kwamba nchi yao ni kama nchi ambayo haijanyeshewa mvua, imenyauka kwa sababu ya ghadhabu yangu ikawa kama ardhi bila maji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mwanadamu, iambie nchi, ‘Wewe ni nchi ambayo haijatakaswa wala kunyeshewa katika siku ya ghadhabu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanadamu, uiambie nchi, Wewe u nchi isiyosafika, wala kunyeshewa mvua siku ya ghadhabu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wewe mtu! Waambie Waisraeli kwamba nchi yao ni kama nchi ambayo haijanyeshewa mvua, imenyauka kwa sababu ya ghadhabu yangu ikawa kama ardhi bila maji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mwanadamu, iambie nchi, ‘Wewe ni nchi ambayo haijapata mvua wala manyunyu katika siku ya ghadhabu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mwanadamu, iambie nchi, ‘Wewe ni nchi ambayo haijapata mvua wala manyunyu katika siku ya ghadhabu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanadamu, uiambie nchi, Wewe u nchi isiyotakasika, wala kunyeshewa mvua siku ya ghadhabu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wewe mtu! Waambie Waisraeli kwamba nchi yao ni kama nchi ambayo haijanyeshewa mvua, imenyauka kwa sababu ya ghadhabu yangu ikawa kama ardhi bila maji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwana wa mtu, iambie nchi hii: Wewe ndiwe nchi isiyotakasika, isiyonyweshwa mvua siku ya kukasirikiwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanadamu, uiambie nchi, Wewe u nchi isiyosafika, wala kunyeshewa mvua siku ya ghadhabu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe mwanadamu! Uwaambie Waisraeli kwamba inchi yao ni kama inchi ambayo haijanyeshewa, imenyauka kwa sababu ya kasirani yangu ikakuwa kama udongo bila maji.