Ezekiel 22:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakuu wenu ni kama simba anayenguruma araruapo mawindo yake. Wanaua watu, wanawanyanganya watu mali na johari, na kuongeza idadi ya wajane.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuna hila mbaya ya wakuu ndani yake kama simba angurumaye akirarua mawindo yake, wanakula watu, wanachukua hazina na vitu vya thamani na kuongeza idadi ya wajane ndani yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Fitina ya manabii wake imo ndani yake, kama simba angurumaye akirarua mawindo; wamekula roho za watu; hutwaa kwa nguvu hazina na vitu vya thamani; wameongeza hesabu ya wajane wake ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakuu wenu ni kama simba anayenguruma araruapo mawindo yake. Wanaua watu, wanawanyang'anya watu mali na johari, na kuongeza idadi ya wajane.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuna hila mbaya ya wakuu ndani yake kama simba angurumaye akirarua mawindo yake, wanakula watu, wanachukua hazina na vitu vya thamani na kuongeza idadi ya wajane ndani yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuna hila mbaya ya wakuu ndani yake kama simba angurumaye akirarua mawindo yake, wanakula watu, wanachukua hazina na vitu vya thamani na kuongeza idadi ya wajane ndani yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Fitina ya manabii wake imo ndani yake, kama simba angurumaye akirarua mawindo; wamekula roho za watu; hutwaa kwa nguvu hazina na vitu vya thamani; wameongeza idadi ya wajane wake ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakuu wenu ni kama simba anayenguruma araruapo mawindo yake. Wanaua watu, wanawanyanganya watu mali na johari, na kuongeza idadi ya wajane.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wafumbuaji wake waliomo mwake wamekula njama, wakawa kama simba angurumaye akinyafua nyama, aliowakamata; nao wakazila roho za watu, wakazitwaa nazo mali zao na vitu vyao vyenye kiasi, wakawaua waume wao wanawake wengi waliokuwamo, wakawageuza kuwa wajane.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Fitina ya manabii wake imo ndani yake, kama simba angurumaye akirarua mawindo; wamekula roho za watu; hutwaa kwa nguvu hazina na vitu vya thamani; wameongeza hesabu ya wajane wake ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa wenu ni kama simba anayenguruma anaporarua nyama wake. Wanaua watu, wanawanyanganya watu mali na vitu vyao vya bei kali, na kuongeza hesabu ya wajane.