Ezekiel 22:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Manabii wake wanaficha maovu hayo kama mtu anapotia chokaa kwenye ukuta mbovu. Wanaona maono ya uongo na kutabiri udanganyifu mtupu, wakisema, ‘Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi,’ wakati mimi mwenyewe sijawaambia chochote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Manabii wake wanapaka chokaa matendo haya kwa maono ya uongo na utabiri wa udanganyifu. Wanasema, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi,’ wakati Mwenyezi Mungu hajasema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na manabii wake wamewapakia chokaa isiyokorogwa vema, wakiona ubatili, na kuwatabiria maneno ya uongo, wakisema, Bwana MUNGU asema hivi; iwapo Bwana hakusema neno.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Manabii wake wanaficha maovu hayo kama mtu anapotia chokaa kwenye ukuta mbovu. Wanaona maono ya uongo na kutabiri udanganyifu mtupu, wakisema, ‘Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi,’ wakati mimi mwenyewe sijawaambia chochote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Manabii wake wanapaka chokaa matendo haya kwa maono ya uongo na utabiri wa udanganyifu. Wanasema, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo,’ wakati BWANA hajasema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Manabii wake wanapaka chokaa matendo haya kwa maono ya uongo na utabiri wa udanganyifu. Wanasema, ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo,’ wakati bwana hajasema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na manabii wake wamewapakia chokaa isiyokorogwa vema, wakiwa na maono ya udanganyifu, na kuwatabiria maneno ya uongo, wakisema, Bwana MUNGU asema hivi; iwapo BWANA hakusema neno.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Manabii wake wanaficha maovu hayo kama mtu anapotia chokaa kwenye ukuta mbovu. Wanaona maono ya uongo na kutabiri udanganyifu mtupu, wakisema, ‘Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi,’ wakati mimi mwenyewe sijawaambia chochote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wafumbuaji wake huyapaka mambo yao yote chokaa, wakiona maono ya uwongo na kusema: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema, naye Bwana hakusema neno.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na manabii wake wamewapakia chokaa isiyokorogwa vema, wakiona ubatili, na kuwatabiria maneno ya uongo, wakisema, Bwana MUNGU asema hivi; iwapo BWANA hakusema neno.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Manabii wake wanaficha maovu hayo kama mutu anapotia chokaa kwenye ukuta wenye kuharibika. Wanapata maono ya uongo na kutabiri udanganyifu mutupu, wakisema “Bwana wetu Yawe anasema hivi”, wakati mimi mwenyewe sikuwaambia chochote.