Ezekiel 22:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mahali nchini ni dhuluma na unyanganyi. Wanawadhulumu maskini na wanyonge, na kuwaonea wageni bila kujali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wa nchi wanatoza kwa nguvu na kufanya unyang’anyi, wanawadhulumu maskini na wahitaji, na kuwaonea wageni, wakiwanyima haki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wa nchi wametumia udhalimu, wamenyang'anya kwa nguvu; naam, wamewatenda jeuri maskini na wahitaji, nao wamewaonea wageni bila haki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mahali nchini ni dhuluma na unyang'anyi. Wanawadhulumu maskini na wanyonge, na kuwaonea wageni bila kujali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wa nchi wanatoza kwa nguvu na kufanya unyang'anyi, wanawatenda jeuri maskini na wahitaji na kuwaonea wageni, wakiwanyima haki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa nchi wanatoza kwa nguvu na kufanya unyang’anyi, wanawatenda jeuri maskini na wahitaji na kuwaonea wageni, wakiwanyima haki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wa nchi wametumia udhalimu, wamenyang'anya kwa nguvu; naam, wamewatenda jeuri maskini na wahitaji, nao wamewaonea wageni bila haki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mahali nchini ni dhuluma na unyanganyi. Wanawadhulumu maskini na wanyonge, na kuwaonea wageni bila kujali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wa nchi hii hukorofisha kabisa na kupokonya sana, hutesa wanyonge na wakiwa, hukorofisha nao wageni kwa njia zisizonyoka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wa nchi wametumia udhalimu, wamenyang’anya kwa nguvu; naam, wamewatenda jeuri maskini na wahitaji, nao wamewaonea wageni bila haki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila fasi katika inchi watu wanatendeana vibaya na kunyanganya kwa kinguvu. Wanagandamiza wamasikini na wakosefu, na kuwaonea wageni bila kujali.