Ezekiel 22:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Una hatia kutokana na damu uliyomwaga. Umejifanya najisi kwa sanamu ulizojifanyia. Siku yako ya adhabu umeileta karibu nawe; naam, siku zako zimehesabiwa. Ndio maana nimekufanya udhihakiwe na mataifa na kudharauliwa na nchi zote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
umekuwa na hatia kwa sababu ya damu uliyomwaga, na umetiwa unajisi kwa sanamu ulizotengeneza. Umejiletea mwisho wa siku zako na mwisho wa miaka yako umewadia. Kwa hiyo nitakufanya kitu cha kudharauliwa kwa mataifa na kitu cha mzaha kwa nchi zote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Umekuwa na hatia katika damu yako uliyomwaga, nawe umekuwa na unajisi kwa vinyago vyako ulivyovifanya; nawe umezileta karibu siku zako, nawe umefika karibu na miaka yako; basi, kwa sababu ya hayo, nimekufanya kuwa lawama kwa mataifa, na kuwa dhihaka katika nchi zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Una hatia kutokana na damu uliyomwaga. Umejifanya najisi kwa sanamu ulizojifanyia. Siku yako ya adhabu umeileta karibu nawe; naam, siku zako zimehesabiwa. Ndio maana nimekufanya udhihakiwe na mataifa na kudharauliwa na nchi zote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
umekuwa na hatia kwa sababu ya damu uliyomwaga na umetiwa unajisi kwa sanamu ulizotengeneza. Umejiletea mwisho wa siku zako na mwisho wa miaka yako umewadia. Kwa hiyo nitakufanya kitu cha kudharauliwa kwa mataifa na kitu cha mzaha kwa nchi zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
umekuwa na hatia kwa sababu ya damu uliyomwaga na umetiwa unajisi kwa sanamu ulizotengeneza. Umejiletea mwisho wa siku zako na mwisho wa miaka yako umewadia. Kwa hiyo nitakufanya kitu cha kudharauliwa kwa mataifa na kitu cha mzaha kwa nchi zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Umekuwa na hatia katika damu yako uliyomwaga, nawe umekuwa na unajisi kwa vinyago vyako ulivyovifanya; nawe umezileta karibu siku zako, nawe umefika karibu na miaka yako; basi, kwa sababu ya hayo, nimekufanya kuwa lawama kwa mataifa, na kuwa dhihaka katika nchi zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Una hatia kutokana na damu uliyomwaga. Umejifanya najisi kwa sanamu ulizojifanyia. Siku yako ya adhabu umeileta karibu nawe; naam, siku zako zimehesabiwa. Ndio maana nimekufanya udhihakiwe na mataifa na kudharauliwa na nchi zote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hizo damu zako, ulizozimwaga, umekora manza, tena kwa hayo magogo ya kutambikia, uliyoyafanya, umejipatia uchafu, hivyo umezifikisha siku zako karibu, ukaja penye mwisho wa miaka yako. Kwa hiyo nitakutia soni kwa wamizimu, usimangwe katika nchi zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Umekuwa na hatia katika damu yako uliyomwaga, nawe umekuwa na unajisi kwa vinyago vyako ulivyovifanya; nawe umezileta karibu siku zako, nawe umefika karibu na miaka yako; basi, kwa sababu ya hayo, nimekufanya kuwa lawama kwa mataifa, na kuwa dhihaka katika nchi zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Una makosa kutokana na damu uliyomwanga. Umejichafua kwa sanamu ulizojifanyia. Umeileta siku yako ya azabu karibu nawe; siku zako zimehesabiwa. Ndiyo maana nimekufanya uchekelewe na mataifa na kuzarauliwa na inchi zote.