Ezekiel 23:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nami nitakuelekezea ghadhabu yangu, nao watakutenda kwa hasira kali. Watakukata pua na masikio na watu wako watakaosalia watauawa kwa upanga. Watawachukua watoto wako wa kiume na wa kike, na watu wako watakaosalia watateketezwa kwa moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitaelekeza hasira yangu yenye wivu dhidi yako, nao watakuadhibu kwa hasira kali. Watakatilia mbali pua yako na masikio yako, na wale watakaosalia miongoni mwako watauawa kwa upanga. Watachukua wana wako wa kiume na wa kike, na wale watakaosalia miongoni mwenu watateketezwa kwa moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitaweka wivu wangu juu yako, nao watakutenda mambo kwa ghadhabu; watakuondolea pua yako na masikio yako; na mabaki yako wataanguka kwa, upanga; watawatwaa wanao na binti zako; na mabaki yako watateketea motoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nami nitakuelekezea ghadhabu yangu, nao watakutenda kwa hasira kali. Watakukata pua na masikio na watu wako watakaosalia watauawa kwa upanga. Watawachukua watoto wako wa kiume na wa kike, na watu wako watakaosalia watateketezwa kwa moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitaelekeza wivu wa hasira yangu dhidi yako nao watakushughulikia kwa hasira kali. Watakatilia mbali pua yako na masikio yako, na wale watakaosalia miongoni mwako watauawa kwa upanga. Watachukua wana wako na binti zako na wale watakaosalia miongoni mwenu watateketezwa kwa moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitaelekeza wivu wa hasira yangu dhidi yako, nao watakushughulikia kwa hasira kali. Watakatilia mbali pua yako na masikio yako, na wale watakaosalia miongoni mwako watauawa kwa upanga. Watachukua wana wako na binti zako, na wale watakaosalia miongoni mwenu watateketezwa kwa moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitaweka wivu wangu juu yako, nao watakutenda mambo kwa ghadhabu; watakuondolea pua yako na masikio yako; na mabaki yako wataanguka kwa upanga; watawatwaa wanao na binti zako; na mabaki yako watateketea motoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nami nitakuelekezea ghadhabu yangu, nao watakutenda kwa hasira kali. Watakukata pua na masikio na watu wako watakaosalia watauawa kwa upanga. Watawachukua watoto wako wa kiume na wa kike, na watu wako watakaosalia watateketezwa kwa moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nitakutolea wivu wangu, wao wakufanyizie mambo, wayatakayo kwa makali yao yenye moto; watakukata pua na masikio, kisha utauawa kwa upanga. Kisha watawachukua wanao wa kiume na wa kike, nawe wewe mwisho utateketezwa kwa moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitaweka wivu wangu juu yako, nao watakutenda mambo kwa ghadhabu; watakuondolea pua yako na masikio yako; na mabaki yako wataanguka kwa, upanga; watawatwaa wanao na binti zako; na mabaki yako watateketea motoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nami nitakuelekezea kasirani yangu, nao watakutendea kwa hasira kali. Watakukata pua na masikio na watu wako watakaobaki watauawa kwa upanga. Watawatwaa wana na wabinti zako, na watu wako watakaobaki watateketezwa kwa moto.