Ezekiel 23:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule mkubwa aliitwa Ohola, na yule mdogo Oholiba. Basi, wote wakawa wangu, wakanizalia watoto, wa kiume na wa kike. Basi, Ohola ni Samaria na Oholiba ni Yerusalemu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkubwa aliitwa Ohola, na mdogo wake Oholiba. Walikuwa wangu nao wakazaa watoto wa kiume na wa kike. Ohola ni Samaria, Oholiba ni Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na majina yao, mkubwa aliitwa Ohola, na umbu lake Oholiba; wakawa wangu, wakazaa wana na binti. Na katika hayo majina yao, Samaria ni Ohola, na Yerusalemu ni Oholiba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule mkubwa aliitwa Ohola, na yule mdogo Oholiba. Basi, wote wakawa wangu, wakanizalia watoto, wa kiume na wa kike. Basi, Ohola ni Samaria na Oholiba ni Yerusalemu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkubwa aliitwa Ohola na mdogo wake Oholiba. Walikuwa wangu nao wakazaa wavulana na msichana. Ohola ni Samaria, Oholiba ni Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mkubwa aliitwa Ohola na mdogo wake Oholiba. Walikuwa wangu nao wakazaa wavulana na msichana. Ohola ni Samaria, Oholiba ni Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na majina yao, mkubwa aliitwa Ohola, na dada yake Oholiba; wakawa wangu, wakazaa watoto wa kiume na wa kike. Na katika hayo majina yao, Samaria ni Ohola, na Yerusalemu ni Oholiba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule mkubwa aliitwa Ohola, na yule mdogo Oholiba. Basi, wote wakawa wangu, wakanizalia watoto, wa kiume na wa kike. Basi, Ohola ni Samaria na Oholiba ni Yerusalemu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Majina yao mkubwa aliitwa Ohola (Hema lake) naye nduguye Oholiba (Hema langu limo mwake); wakawa wangu, wakazaa wana wa kiume na wa kike. Nayo hayo majina yao lile la Ohola lilikuwa la Samaria, nalo la Oholiba lilikuwa la Yerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na majina yao, mkubwa aliitwa Ohola, na umbu lake Oholiba; wakawa wangu, wakazaa wana na binti. Na katika hayo majina yao, Samaria ni Ohola, na Yerusalemu ni Oholiba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mukubwa aliitwa Ohola, na yule mudogo Oholiba. Basi, wote wakakuwa wangu, wakanizalia watoto, wana na wabinti. Basi, Ohola ni Samaria na Oholiba ni Yerusalema!