Ezekiel 23:40 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Hata walituma wajumbe wawaite watu wa mbali, nao wakaja. Kwa ajili yao, walioga, wakajitia wanja na kujipamba kwa johari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hata waliwatuma wajumbe kuwaita watu kutoka mbali, nao walipowasili ulioga kwa ajili yao, ukapaka macho yako wanja, na ukavaa mapambo yako yaliyotengenezwa kwa vito vya dhahabu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mmewatuma watu kuwaita watokao mbali; ambao mjumbe alitumwa kwao, na tazama, wakaja; nawe ulijiosha kwa ajili yao, ulitia rangi macho yako, na kujipamba vyombo vya uzuri;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Hata walituma wajumbe wawaite watu wa mbali, nao wakaja. Kwa ajili yao, walioga, wakajitia wanja na kujipamba kwa johari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Walituma hata wajumbe kuwaita watu kutoka mbali, nao walipowasili ulioga kwa ajili yao, ukapaka macho yako rangi na ukavaa mapambo yako yaliyotengenezwa kwa vito vya dhahabu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Walituma hata wajumbe kuwaita watu kutoka mbali, nao walipowasili ulioga kwa ajili yao, ukapaka macho yako rangi na ukavaa mapambo yako yaliyotengenezwa kwa vito vya dhahabu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mmewatuma watu kuwaita watokao mbali; ambao mjumbe alitumwa kwao, na tazama, wakaja; nawe ulijiosha kwa ajili yao, ulitia rangi macho yako, na kuremba kwa mapambo mazuri;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Hata walituma wajumbe wawaite watu wa mbali, nao wakaja. Kwa ajili yao, walioga, wakajitia wanja na kujipamba kwa johari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena wametuma hata kwa waume walioko mbali, waje wakitoka kwao; nao hapo, mjumbe alipotumwa kuwaita, ndipo, walipokuja papo hapo. Kwa ajili yao ukaenda koga, ukajitia wanja machoni, ukajipamba na kuvaa mapambo ya urembo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mmewatuma watu kuwaita watokao mbali; ambao mjumbe alitumwa kwao, na tazama, wakaja; nawe ulijiosha kwa ajili yao, ulitia rangi macho yako, na kujipamba vyombo vya uzuri;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata walituma wajumbe wawaite watu wa mbali, nao wakakuja. Kwa ajili yao, walikoga, wakajitia wanja na kuvaa vitu vya kujipamba.