Ezekiel 24:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utasononeka, lakini sio kwa sauti. Hutamfanyia matanga huyo aliyekufa. Vaa viatu vyako na kuvaa kilemba; usiufunike uso wako wala kula chakula cha matanga.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lia kwa uchungu kimya kimya usimwombolezee mtu aliyekufa. Jifunge kilemba chako na uvae viatu vyako miguuni mwako, usifunike sehemu ya chini ya uso wako, wala usile vyakula vya waombolezaji.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ugua lakini si kwa sauti ya kusikiwa; usifanye matanga kwa ajili yake yeye aliyekufa; jipige kilemba chako, ukavae viatu vyako, wala usiifunike midomo yako, wala usile chakula cha watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utasononeka, lakini sio kwa sauti. Hutamfanyia matanga huyo aliyekufa. Vaa viatu vyako na kuvaa kilemba; usiufunike uso wako wala kula chakula cha matanga.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lia kwa uchungu kimya kimya usimwombolezee mtu aliyekufa. Jifunge kilemba chako na uvae viatu vyako miguuni mwako, usifunike sehemu ya chini ya uso wako, wala usile vyakula vya kawaida vya wakati wa matanga.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lia kwa uchungu kimya kimya usimwombolezee mtu aliyekufa. Jifunge kilemba chako na uvae viatu vyako miguuni mwako, usifunike sehemu ya chini ya uso wako, wala usile vyakula vya kawaida vya wakati wa matanga.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Piga kite lakini si kwa sauti ya kusikiwa; usifanye matanga kwa ajili yake yeye aliyekufa; jipige kilemba chako, ukavae viatu vyako, wala usiifunike midomo yako, wala usile chakula cha watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utasononeka, lakini sio kwa sauti. Hutamfanyia matanga huyo aliyekufa. Vaa viatu vyako na kuvaa kilemba; usiufunike uso wako wala kula chakula cha matanga.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Piga kite usiposikiwa; lakini aliyekufa usimfanyizie matanga! jifunge kilemba chako, kavae viatu miguuni pako! Lakini usiufunike udevu wa midomoni, wala usile chakula, watu watakachokuletea!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ugua lakini si kwa sauti ya kusikiwa; usifanye matanga kwa ajili yake yeye aliyekufa; jipige kilemba chako, ukavae viatu vyako, wala usiifunike midomo yako, wala usile chakula cha watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utaugua, lakini sio kwa sauti. Hautamufanyia kilio huyo aliyekufa. Vaa viatu vyako na kuvaa kitambaa; usiufunike uso wako wala kula chakula cha kilio.