Ezekiel 24:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
niwaambie nyinyi Waisraeli kwamba Mwenyezi-Mungu ataitia unajisi maskani yake, hiyo nyumba ambayo ni fahari ya ukuu wenu, na ambayo mnafurahi sana kuiona. Nao watoto wenu, wa kiume kwa wa kike, mliowaacha nyuma watauawa kwa upanga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
‘Sema na nyumba ya Israeli. Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ninakaribia kupatia unajisi mahali pangu patakatifu, ngome ambayo ndani yake mnaona fahari, furaha ya macho yenu, kitu mnachokipenda. Wana wenu wa kiume na wa kike mliowaacha nyuma wataanguka kwa upanga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Angalieni, nitapatia unajisi patakatifu pangu, fahari ya uwezo wenu, mahali pa kutamaniwa na macho yenu, ambapo roho zenu zinapahurumia na wana wenu na binti zenu, mliowaacha nyuma, wataanguka kwa upanga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
niwaambie nyinyi Waisraeli kwamba Mwenyezi-Mungu ataitia unajisi maskani yake, hiyo nyumba ambayo ni fahari ya ukuu wenu, na ambayo mnafurahi sana kuiona. Nao watoto wenu, wa kiume kwa wa kike, mliowaacha nyuma watauawa kwa upanga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
‘Sema na nyumba ya Israeli. Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Ninakaribia kupatia unajisi mahali pangu patakatifu, ngome ambayo ndani yake mnaona fahari, furaha ya macho yenu, kitu mnachokipenda. Wana wenu na binti zenu mliowaacha nyuma wataanguka kwa upanga.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
‘Sema na nyumba ya Israeli. Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Ninakaribia kupatia unajisi mahali pangu patakatifu, ngome ambayo ndani yake mnaona fahari, furaha ya macho yenu, kitu mnachokipenda. Wana wenu na binti zenu mliowaacha nyuma wataanguka kwa upanga.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Angalieni, nitapatia unajisi patakatifu pangu, fahari ya uwezo wenu, mahali pa kutamaniwa na macho yenu, ambapo roho zenu zinapahurumia na wana wenu na binti zenu, mliowaacha nyuma, wataanguka kwa upanga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
niwaambie nyinyi Waisraeli kwamba Mwenyezi-Mungu ataitia unajisi maskani yake, hiyo nyumba ambayo ni fahari ya ukuu wenu, na ambayo mnafurahi sana kuiona. Nao watoto wenu, wa kiume kwa wa kike, mliowaacha nyuma watauawa kwa upanga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uambie mlango wa Isiraeli: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona, nikipapatia uchafu Patakatifu pangu palipo majivuno yenu makuu na tamaa ya macho yenu na upendeleo wa roho zenu. Nao wana wenu wa kiume na wa kike, mliowaacha, wataangushwa kwa panga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Angalieni, nitapatia unajisi patakatifu pangu, fahari ya uwezo wenu, mahali pa kutamaniwa na macho yenu, ambapo roho zenu zinapahurumia na wana wenu na binti zenu, mliowaacha nyuma, wataanguka kwa upanga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uwaambie Waisraeli kwamba: Bwana wetu Yawe anasema hivi: Nitalichafua hekalu langu, hiyo nyumba ambayo munajivunia na kuitegemea na ambao munafurahi sana kuiona.