Ezekiel 25:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
basi, mimi nimeunyosha mkono dhidi yenu; nitawaacha mtekwe nyara na watu wa mataifa mengine. Nitawaangamizeni, nanyi hamtakuwa taifa tena wala kuwa na nchi. Hapo ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
hivyo nitaunyoosha mkono wangu dhidi yenu na kuwatoa kuwa nyara kwa mataifa. Nitawakatilia mbali kutoka mataifa na kuwang’oa kutoka nchi. Nitawaangamiza, nanyi mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
basi, tazama, nimenyosha mkono wangu juu yako, nami nitakutoa uwe mateka ya mataifa; nami nitakukatilia mbali na kabila za watu, nami nitakuangamiza, usiwe katika nchi hizo; nitakukomesha; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
basi, mimi nimeunyosha mkono dhidi yenu; nitawaacha mtekwe nyara na watu wa mataifa mengine. Nitawaangamizeni, nanyi hamtakuwa taifa tena wala kuwa na nchi. Hapo ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
hivyo nitaunyosha mkono wangu dhidi yako na kukutoa kuwa nyara kwa mataifa. Nitakukatilia mbali kutoka kwenye mataifa na kukung'oa katika nchi. Nitakuangamiza, nawe utajua ya kuwa Mimi ndimi BWANA.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
hivyo nitaunyoosha mkono wangu dhidi yako na kukutoa kuwa nyara kwa mataifa. Nitakukatilia mbali kutoka kwenye mataifa na kukung’oa katika nchi. Nitakuangamiza, nawe utajua ya kuwa Mimi ndimi bwana.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
basi, tazama, nimenyosha mkono wangu juu yako, nami nitakutoa uwe mateka ya mataifa; nami nitakukatilia mbali na makabila ya watu, nami nitakuangamiza, usiwe katika nchi hizo; nitakukomesha; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
basi, mimi nimeunyosha mkono dhidi yenu; nitawaacha mtekwe nyara na watu wa mataifa mengine. Nitawaangamizeni, nanyi hamtakuwa taifa tena wala kuwa na nchi. Hapo ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwa hiyo utaniona, nikikukunjulia mkono wangu, nikutolee mataifa mengine, wakunyang'anye, kisha nitakuangamiza kwenye makabila ya watu, nikupoteze na kukutowesha katika nchi hizi. Ndipo, utakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
basi, tazama, nimenyosha mkono wangu juu yako, nami nitakutoa uwe mateka ya mataifa; nami nitakukatilia mbali na kabila za watu, nami nitakuangamiza, usiwe katika nchi hizo; nitakukomesha; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
basi, mimi nimeunyoosha mukono juu yenu kwa kuwaazibu; nitawaacha mukamatwe mateka na watu wa mataifa mengine. Nitawaangamiza kabisa, nanyi hamutakuwa taifa tena wala kuwa na inchi. Kwa hiyo mutatambua kwamba mimi ni Yawe.