Ezekiel 26:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Farasi wa mfalme Nebukadneza ni wengi na vumbi watakalotimua litakufunika. Kuta zako zitatetemeka kwa mshindo wa wapandafarasi na magari ya vita na ya mizigo wakati atakapoingia kwenye malango yako kama watu waingiavyo mjini kupitia mahali palipobomolewa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Farasi wake watakuwa wengi sana kiasi kwamba utafunikwa na mavumbi watakayotimua. Kuta zako zitatikisika kwa mshindo wa farasi wa vita, magari ya kukokotwa, na magari ya vita wakati aingiapo malango yako kama watu wanaoingia mji ambao kuta zake zimebomolewa kote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu wingi wa farasi zake, mavumbi yao yatakufunika; kuta zako zitatetemeka kwa sababu ya mshindo wa wapanda farasi, na wa magurudumu, na wa magari ya vita, atakapoingia katika malango yako, kama watu waingiavyo katika mji uliobomolewa mahali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Farasi wa mfalme Nebukadneza ni wengi na vumbi watakalotimua litakufunika. Kuta zako zitatetemeka kwa mshindo wa wapandafarasi na magari ya vita na ya mizigo wakati atakapoingia kwenye malango yako kama watu waingiavyo mjini kupitia mahali palipobomolewa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Farasi zake zitakuwa nyingi sana kiasi kwamba utafunikwa na mavumbi watakayotimua. Kuta zako zitatikisika kwa mshindo wa farasi wa vita, magari makubwa na magari ya vita wakati aingiapo malango yako kama watu waingiao mji ambao kuta zake zimebomolewa kote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Farasi zake zitakuwa nyingi sana kiasi kwamba utafunikwa na mavumbi watakayotimua. Kuta zako zitatikisika kwa mshindo wa farasi wa vita, magari makubwa na magari ya vita wakati aingiapo malango yako kama watu waingiao mji ambao kuta zake zimebomolewa kote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu wingi wa farasi wake, mavumbi yao yatakufunika; kuta zako zitatetemeka kwa sababu ya mshindo wa wapanda farasi, na wa magurudumu, na wa magari ya vita, atakapoingia katika malango yako, kama watu waingiavyo katika mji uliobomolewa mahali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Farasi wa mfalme Nebukadneza ni wengi na vumbi watakalotimua litakufunika. Kuta zako zitatetemeka kwa mshindo wa wapandafarasi na magari ya vita na ya mizigo wakati atakapoingia kwenye malango yako kama watu waingiavyo mjini kupitia mahali palipobomolewa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kuwa na farasi wengi mavumbi yao yatakufunika, kwa mashindo ya wapanda farasi na za magurudumu na za magari kuta zako zitatetemeka, atakapoingia katika malango yako, kama watu wanavyoingia katika mji uliovunjwa kwa nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu wingi wa farasi zake, mavumbi yao yatakufunika; kuta zako zitatetemeka kwa sababu ya mshindo wa wapanda farasi, na wa magurudumu, na wa magari ya vita, atakapoingia katika malango yako, kama watu waingiavyo katika mji uliobomolewa mahali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Farasi wa mufalme Nebukadneza ni wengi na mavumbi watakayorusha juu yatakufunika. Kuta zako zitatetemeka kwa mushindo wa waaskari wapanda-farasi na magari ya vita na ya mizigo wakati atakapoingia kwenye milango yako kama watu wanavyoingia katika muji kupitia pahali palipobomolewa.