Ezekiel 26:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utajiri wako watauteka pamoja na bidhaa zako. Watazibomoa kuta zako na kuziangusha nyumba zako za fahari; mawe, mbao na udongo ulivyotumia kujengea nyumba hizo watavitupa baharini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watateka utajiri wako na kuchukua nyara bidhaa zako, watazivunja kuta zako na kuzibomoa nyumba zako nzuri, watatupa baharini mawe yako, mbao zako na kifusi chako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wataufanya utajiri wako kuwa mateka, na bidhaa yako kuwa mawindo; nao watazibomoa kuta zako, na kuziharibu nyumba zako zipendezazo; nao wataweka mawe yako, na miti yako, na mavumbi yako, kati ya maji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utajiri wako watauteka pamoja na bidhaa zako. Watazibomoa kuta zako na kuziangusha nyumba zako za fahari; mawe, mbao na udongo ulivyotumia kujengea nyumba hizo watavitupa baharini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watateka utajiri wako na kuchukua nyara bidhaa zako, watazivunja kuta zako na kuzibomoa nyumba zako nzuri, watatupa baharini mawe yako, mbao zako na kifusi chako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watateka utajiri wako na kuchukua nyara bidhaa zako, watazivunja kuta zako na kuzibomoa nyumba zako nzuri, watatupa baharini mawe yako, mbao zako na kifusi chako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wataufanya utajiri wako kuwa mateka, na bidhaa yako kuwa mawindo; nao watazibomoa kuta zako, na kuziharibu nyumba zako zipendezazo; nao watatupa mawe yako, na miti yako, na mavumbi yako, kati ya maji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utajiri wako watauteka pamoja na bidhaa zako. Watazibomoa kuta zako na kuziangusha nyumba zako za fahari; mawe, mbao na udongo ulivyotumia kujengea nyumba hizo watavitupa baharini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vilimbiko vyako watavinyang'anya, nazo mali zako za kuchuuzia wataziteka, kuta zako za boma watazibomoa, majumba yako, uliyoyatamani kwa uzuri wao, watayavunja, kisha watayatupa baharini mawe yako na miti yako na mavumbi yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wataufanya utajiri wako kuwa mateka, na bidhaa yako kuwa mawindo; nao watazibomoa kuta zako, na kuziharibu nyumba zako zipendezazo; nao wataweka mawe yako, na miti yako, na mavumbi yako, kati ya maji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ataunyanganya utajiri wako pamoja na biashara yako. Atazibomoa kuta zako na kuziangusha nyumba zako nzuri; mawe, mbao na udongo ulivyotumia kwa kujenga nyumba hizo watavitupa katika bahari.