Ezekiel 26:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitakufanya kuwa jabali tupu; utakuwa mahali pa wavuvi kukaushia nyavu zao, wala hutajengwa tena. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitakufanya mwamba mtupu, nawe utakuwa mahali pa kutandazia nyavu za kuvulia samaki. Kamwe hutajengwa tena, kwa maana Mimi Mwenyezi Mungu nimenena, asema Bwana Mungu Mwenyezi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitakufanya kuwa jabali tupu; utakuwa mahali pa kutandazia nyavu za wavuvi; hutajengwa tena; maana mimi, Bwana, nimenena neno hili, asema Bwana MUNGU.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitakufanya kuwa jabali tupu; utakuwa mahali pa wavuvi kukaushia nyavu zao, wala hutajengwa tena. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitakufanya mwamba mtupu, nawe utakuwa mahali pa kutandazia nyavu za kuvulia samaki. Kamwe hutajengwa tena, kwa maana Mimi BWANA nimenena, asema BWANA Mwenyezi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitakufanya mwamba mtupu, nawe utakuwa mahali pa kutandazia nyavu za kuvulia samaki. Kamwe hutajengwa tena, kwa maana Mimi bwana nimenena, asema bwana Mwenyezi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitakufanya kuwa jabali tupu; utakuwa mahali pa kutandazia nyavu za wavuvi; hutajengwa tena; maana mimi, BWANA, nimenena neno hili, asema Bwana MUNGU.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitakufanya kuwa jabali tupu; utakuwa mahali pa wavuvi kukaushia nyavu zao, wala hutajengwa tena. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo nitakugeuza kuwa mwamba mtupu, uwe mahali pa kuanikia nyavu, hutajengwa tena, kwani mimi Bwana nimeyasema; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitakufanya kuwa jabali tupu; utakuwa mahali pa kutandazia nyavu za wavuvi; hutajengwa tena; maana mimi, BWANA, nimenena neno hili, asema Bwana MUNGU.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitakufanya kuwa kama jiwe; utakuwa pahali pa wavuvi pa kukaushia nyavu zao, wala hautajengwa tena. Mimi Yawe nimesema. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe.