Ezekiel 26:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakuu wote wa mataifa ya pwani watashuka toka viti vyao vya enzi, na kuvua mavazi yao ya heshima pamoja na nguo zao zilizotariziwa. Wakiwa wamejaa hofu, wataketi chini; nao watatetemeka wakati wote na kushangaa mno juu ya hayo yaliyokupata.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo wakuu wote wa mataifa ya pwani watashuka kutoka viti vyao vya utawala, na kuweka kando majoho yao na kuvua nguo zao zilizotariziwa. Wataketi chini ardhini, wakiwa wamevikwa hofu kuu, wakitetemeka kila dakika na kukustaajabia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo wakuu wote wa bahari watashuka kutoka viti vyao vya enzi, na kuweka upande mavazi yao, na kuvua nguo zao zilizotiwa taraza; watajivika matetemeko; wataketi na kutetemeka kila dakika, na kukustaajabia,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakuu wote wa mataifa ya pwani watashuka toka viti vyao vya enzi, na kuvua mavazi yao ya heshima pamoja na nguo zao zilizotariziwa. Wakiwa wamejaa hofu, wataketi chini; nao watatetemeka wakati wote na kushangaa mno juu ya hayo yaliyokupata.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo wakuu wote wa mataifa ya pwani watashuka kutoka kwenye viti vyao vya enzi na kuweka kando majoho yao na kuvua nguo zao zilizotariziwa. Wakiwa wamevikwa hofu kuu, wataketi chini ardhini, wakiwa wanatetemeka kila dakika na wakikustajabia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo wakuu wote wa mataifa ya pwani watashuka kutoka kwenye viti vyao vya enzi na kuweka kando majoho yao na kuvua nguo zao zilizotariziwa. Wakiwa wamevikwa hofu kuu, wataketi chini ardhini, wakiwa wanatetemeka kila dakika na wakikustajabia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo wakuu wote wa bahari watashuka kutoka viti vyao vya enzi, na kuweka upande mavazi yao, na kuvua nguo zao zilizotiwa tarizi; watajivika wakitetemeka; wataketi na kutetemeka kila dakika, na kukustaajabia,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakuu wote wa mataifa ya pwani watashuka toka viti vyao vya enzi, na kuvua mavazi yao ya heshima pamoja na nguo zao zilizotariziwa. Wakiwa wamejaa hofu, wataketi chini; nao watatetemeka wakati wote na kushangaa mno juu ya hayo yaliyokupata.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wafalme wote wa nchi zilizoko baharini watashuka katika viti vyao vya kifalme wakiziondoa kanzu zao za urembo na kuzivua nazo nguo zao za rangi, kisha watajivika mastuko na kukaa chini, wakistuka mara kwa mara kwa kupigwa na bumbuazi kwa ajili yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo wakuu wote wa bahari watashuka kutoka viti vyao vya enzi, na kuweka upande mavazi yao, na kuvua nguo zao zilizotiwa taraza; watajivika matetemeko; wataketi na kutetemeka kila dakika, na kukustaajabia,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa wote wa mataifa ya kandokando ya bahari watashuka toka kwenye viti vyao vya kifalme, na kuvua nguo zao za heshima pamoja na nguo zao zilizopindwa. Kisha kujaa hofu, wataikaa chini; nao watatetemeka wakati wote na kushangaa sana juu ya hayo yaliyokupata.