Ezekiel 26:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wataimba utenzi huu wa kuomboleza: Umeangamizwa wewe mji maarufu, umetoweka kutoka baharini! Wakazi wake walieneza nguvu zao juu ya bahari, ambapo walihofiwa na wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo wao watakuombolezea na kukuambia: “ ‘Tazama jinsi ulivyoharibiwa, ee mji uliokuwa na sifa, wewe uliyekaliwa na mabaharia! Ulikuwa na nguvu kwenye bahari, wewe na wakaaji wako; wote walioishi huko, uliwatia hofu kuu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watakufanyia maombolezo, na kukuambia, Imekuwaje wewe kuharibika, wewe uliyekaliwa na wana-maji, mji wenye sifa, uliyekuwa na nguvu katika bahari, mji huo, na hao waliokaa ndani yake, waliowatia hofu wote waliokaa ndani yake!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wataimba utenzi huu wa kuomboleza: Umeangamizwa wewe mji maarufu, umetoweka kutoka baharini! Wakazi wake walieneza nguvu zao juu ya bahari, ambapo walihofiwa na wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo wao watakuombolezea na kukuambia: “ ‘Tazama jinsi ulivyoharibiwa, Ee mji uliokuwa na sifa, wewe uliyekaliwa na mabaharia! Ulikuwa na nguvu kwenye bahari, wewe na watu wako; wote walioishi huko, uliwatia hofu kuu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo wao watakuombolezea na kukuambia: “ ‘Tazama jinsi ulivyoharibiwa, ee mji uliokuwa na sifa, wewe uliyekaliwa na mabaharia! Ulikuwa na nguvu kwenye bahari, wewe na watu wako; wote walioishi huko, uliwatia hofu kuu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watakufanyia maombolezo, na kukuambia, Imekuwaje wewe kuharibika, wewe uliyekaliwa na wanamaji, mji wenye sifa, uliyekuwa na nguvu katika bahari, mji huo, na hao waliokaa ndani yake, waliowatia hofu wote waliokaa ndani yake!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wataimba utenzi huu wa kuomboleza: Umeangamizwa wewe mji maarufu, umetoweka kutoka baharini! Wakazi wake walieneza nguvu zao juu ya bahari, ambapo walihofiwa na wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha watakutungia ombolezo la kukulilia kwamba: kumbe umeangamia uliokaa baharini, uliokuwa mji wa kusifiwa tu kwa kukaa na nguvu zake baharini, huo wenyewe na watu wake waliokuwamo waliowatisha wote waliokaa pwani kwao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watakufanyia maombolezo, na kukuambia, Imekuwaje wewe kuharibika, wewe uliyekaliwa na wana-maji, mji wenye sifa, uliyekuwa na nguvu katika bahari, mji huo, na hao waliokaa ndani yake, waliowatia hofu wote waliokaa ndani yake!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watakuimbia wimbo huu wa kuomboleza: Namna gani wewe muji wenye utukufu, umetoweka kutoka katika bahari! Ulikuwa na nguvu juu ya bahari, wewe pamoja na wakaaji wako, wewe uliyeletea woga juu ya wote!